Header Ads Widget

NJOMBE MPIRA WA MIGUU USICHEZWE MDOMONI BALI UCHEZWE KIWANJANI.

Rai hiyo imetolewa na Hans Luwanja Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa Miguu Wilaya ya Njombe ( NJODFA) wakati akikabidhi mchango wa sh.300,000 (laki tatu) kwa Uongozi wa timu ya Mbeya road fc (Watoto wa Nyumbani Makambako) kutoka kwa Mjumbe wa mkutano mkuu TFF na Mjumbe wa kamati ya fedha TFF Evance  Mgeusa .  mwandishi wa matukio daima Frederick Siwale anaripoti kutokea Njombe

Luwanja alisema fedha hizo zimetolewa na Mgeusa Kama mdau wa soka Wilaya na Mkoa wa Njombe kwa lengo la kuwapa hamasa timu ya Mbeya road fc ambayo imefikia hatua ya fainali ligi ya mkoa wa Njombe ambayo itafanyika Novemba 23 Jumanne hii katika Uwanja wa Tandala Ikonda Wilayani Makete.                             

Luwanja alisema mkoa wa Njombe inaonekana kuwa nyuma kimichezo chanzo ikiwa ni mchezo wa mpira wa Miguu kuchezwa zaidi mdomoni kuliko kiwanjani  na ndiyo.          

"Mwandishi wa habari wa Matukio Daima tv unaweza kuona ndiyo maana ukanda huu wa mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma hakuna timu iliyoko ligi kuu Kama wenzetu mkoa jirani wa Mbeya ,chanzo  kila mtu ni Kocha na kila mtu mpira anaujua ".Alisema Luwanja.        

Ufike wakati tuache maneno na porojo au propaganda zisizo na tija kwenye mpira na ikiwezekana Njombe tuwe na timu nyingi nyingi katika madaraja tofauti tofauti badala ya kuangalia timu moja peke yake.                

Upande wake Katibu mtendaji wa timu ya Mbeya road fc Godfrey Mwakasita alishukuru msaada huo wa fedha kutoka kwa mdau Evance Mgeusa na kuwaomba wadau wengine wa soka kutoa michango kwa ajili ya kuboresha na kukuza mchezo wa mpira wa Miguu Wilaya na Mkoa wa Njombe.                               

Aidha Mwakasita alilaani tabia mbaya ya baadhi ya Viongozi wanaohusika na michezo kutumia vibaya madaraka yao na sheria na kanuni kudidimiza michezo.        

"Mwandishi wa habari mfano timu hii ya Mbeya road fc yenye Makao makuu yake stendi ya mabasi Makambako katika Halmashauri ya Mji Makambako ambao Safari hii tumekusudia kufanya mageuzi katika soka Mkoani Njombe lakini tunafanyiwa figisu acha kabisa." Alisema Mwakasita.

Alisema mwaka huu Mbeya road fc imeingia kucheza ligi ngazi ya mkoa daraja la tatu Taifa ambapo kituo kilikuwa Uwanja wa Amani Makambako na baada ya kufuzu nane bora ikaonekana michuano inahamia Wilayani Makete badala ya kuchezewa Mkoani.         

Katika maamuzi hayo timu tano za Makambako hearos fc, Chai fc, Zamaleki fc ,Polisi Fc na Mbeya road fc ziligomea kwenda Makete kwa kudai ni kuongezewa gharama za uendeshaji ili hali timu hizo zinajiendesha kwa kutumia michango ya wadau.          

"Tuliandika barua kwa Mwenyekiti wa michezo mkoa wa Njombe ( RAS) ambapo suala letu lilifika kwa afisa Utamaduni na mwisho tukalazimika kwenda kucheza Tandala Ikonda nje kidogo ya Mji wa Makete ,kwa madai kuwa uwanja huo unaunafuu kidogo" Alisema Mwakasita.                        

Alisema ratiba iliyotolewa na Chama cha mpira wa Miguu mkoa wa Njombe NJOREFA inaonyesha fainali ni Tandala lakini baada ya Mbeya road fc kuingia fainali ikiwa imebakia siku moja fainali kufanyika zinakuja taarifa kwa njia ya mdomo kuwa fainali ni Makete Mjini hivi gharama za kuhamisha Wachezaji zinalipwa na nani ? na sababu za kuhamisha fainali ni kitu gani ? Alihoji Mwakasita.               

Post a Comment

1 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI