Watu wenye ulemavu wamekuwa wakipewa kipaumbele na Serikali pamoja na taasisi binafsi katika kuwajengea uwezo wa kitaaluma na hata kuwapa nafasi katika ofisi na wengine kujiajiri wenyewe kutokana na kuwa na weledi,Mwandishi Adrian Audax - MDTV anaripoti kutoka Mwanza
Katika kiliangazia swala hilo Serikali imetoa Kiasi cha shilingi Bil. 8 kwa ajili ya kujenga vyuo viwili pamoja na kukarabati vyuo 6 kwa ajili ya watu wenye ulemavu Mkoani Mwanza,
Akizungumza katika ziara ya kikazi Wilayani Nyamagana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenesta Mhagama amesema kuwa Wizara yake imepokea Shilingi Bil. 8 ili kukarabati vyuo na kujenga vyuo vipya viwili kwa ajili ya Walemavu,
Akiwa katika Chuo cha Ufundi Mirongo kilichopo wilayani Nyamagana ametoa shukurani zake kwa Taasisi ya Desk and Chair Foundation kwa kusaidia kuchimba kisima, Kujenga vyoo pamoja na Kuwafadhili ada wanafunzi 15,
Katika fedha zilizotengwa, Jumla ya Shilingi Millioni 900 zitapelekwa katika Chuo cha Ufundi Mirongo na kutumika katika Ujenzi wa Bweni, Kukarabati Majengo, Karakana pamoja na kununua vifaa vya kufundishia, Amesema Mhagama,
Chuo cha Ufundi Mirongo kilianzishwa mnamo waka 1982 na Halimashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya kuwapa elimu walemavu ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuwajengea stadi za maisha,
0 Comments