Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Urua kijiji cha Mfuruashe wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ambae ni mshereheshaji (MC) maarufu Augustine Moshi (35) atuhumiwa kumuua mkewe Anastasia Augustine (31) kwa kumkatakata na kitu chenye ncha kali kabla ya yeye mwenyewe kuchukua uamuzi wa kujinyonga kutokana na kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.
Imeelezwa kuwa mwenyekiti huyo ambae pia ni MC maarufu katika wilayani Rombo anadaiwa kutenda unyama huo usiku wa kuamkia Novemba 8 mwaka huu 2021.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hil,o mkuu wa wilaya ya Rombo ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Kanali Hamis Maiga alisema kuwa wanandoa hao walikuwa na mgogoro wa kimapenzi ambapo wiki moja iliyopita mke alipeleka malalamiko yake dawati la jinsia wilaya ya Rombo .
Baadhi ya wananchi wa kitongoji hiyo akiwemo Amina Ally walieleza kusikitishwa na tukio hilo na kuwa hata kama mmoja wapo alikuwa na tatizo katika ndoa dawa haikuwa ni kuchukua uamuzi kama huo bali walipaswa kumaliza tofauti zao nje ya maamuzi hayo .
0 Comments