MJADALA WAZIRI WA NISHATI, MHE JANUARY MAKAMBA (MB) UTEUZI WA BODI YA TANESCO NILICHOJIFUNZA WANATAKIWA KUFANYA MAMBO SABA (07) ILI KUPINDUA MEZA
Na.
MwL. Cleopa E. Soi
NDOTO KUBWA
Masijala
Kama kuna mashirika ya umma ambayo yamebakia kama moyo wa nchi, ambayo taifa linapaswa kuyasimamia kwa nguvu na uwezo wake wote na uzalendo ni pamoja na:- 1.Shirika la Umeme Tanesco,
2. Mamlaka ya Bandari,
3. Shirika la Reli, na
4. Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dawasa.
Ni hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alifanya uteuzi mpya wa Waziri na Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO na kwa mamlaka aliyopewa kisheria, Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba (MB) naye akateua wajumbe wapya wa Bodi Habari ikawa kitendo cha bodi hiyo kujumuisha wafanya biashara imeibua mijadala kutokana na jambo hilo jipya baada ya kuona wafanyabiashara wakina comrade Christopher Mwita Gachuma ambaye licha ya biashara ni mwanasiasa kwani amewahi kuwa mjumbe wa Halmashauri kuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa na wengine katika bodi hiyo ni pamoja na Mr. Abubakary Bahresa na Mhe Balozi Mwanaidi Majaar na wengine. Hoja zikajengwa kwa kuwa ni wafanyabiashara na wengine Wana kampuni za Uwakili wangeachwa. Prof. Shivji naye hakubaki nyuma katika mjadala huo naye akajitokeza akajenga hoja wafanyabiashara kutokuwa sehemu ya shirika.
Mijadala mingi inayokosoa kwa hoja imeshindwa kuona Nguvu ya hoja katika hotuba ya Mhe. January Makamba kwa bodi Mpya ya TANESCO ambapo amelitaka Shirika hilo ijiendeshe kwa faida. Ni kweli miaka mingi Shirika hili limekuwa likijiendesha kwa hasara na hata Mhe Zitto Kabwe-ACT yeye amejenga hoja kwa kuonyesha namba jinsi Shirika limekuwa likijiendesha kwa hasara kwa muda mrefu na haja Shirika hili likijiendesha kwa faida.
Inawezekana wengi wanaomkosoa Mhe January Makamba ni kutokana na kutomfahamu ieleweke kwamba ni kati ya Kijana anayejua anawakilisha wengi katika dhamana aliyopewa zaidi sana amejaliwa moyo wa kupenda kuwatumikia watu na ni miongoni mwa Vijana wanaojua changamoto za Shirika la TANESCO akiwa serikalini, Bungeni na akiwa mtumiaji wa huduma ya umeme.
Kuna haja tukawa na mtazamo chanya kwake, Mkurugenzi Mkuu na Bodi Mpya *tukawakopesha Imani, Upendo tukawadai huduma bora.* Nishati ni mahali tunawatarajia watapenda wakumbukwe kwa historia njema na iliyotukuka na zaidi sana kuendeleza kazi njema iliyowekwa na watangulizi wao awamu ya tano.
Sijakosa IMANI, UPENDO NA HATA KUAMINI TUTAONA UWEZA ZAIDI (MIUJIZA) kwa wateule hawa ambao wamewahi beba interest za familia wakaziacha wakabeba za Makampuni yao wakahudumia Jamii na sasa wanaacha interest zao katika biashara wanabeba Maslahi ya Taifa kwa kupitia Shirika hili muhimu katika huduma na Uchumi wa nchi. Kuaminiwa na Taifa na Mhe Rais na Waziri ninaamini kwao ni dhamana kubwa sana.
Tuwakopeshe Imani watupe Uweza wao wanaouonyesha katika biashara maana ni nyakati wao kusukumwa na maslahi ya taifa letu yaliyo makubwa kuliko Maslahi yao, biashara na kampuni zao na kutambua dhamana kubwa waliyokabidhiwa.
Najua wanajua TANESCO ikiyumba, maana yake uchumi wa nchi umeyumba, Usalama wa nchi uko mashakani.
Waziri wa Nishati Mhe January Makamba kuteua wafanya biashara kuongoza TANESCO nadhani ni kutokana na Sera ya Shirika kujiendesha kibiashara inahitaji watu ambao nao wanaelewa biashara ili kuleta tija.
Nchi za Wenzetu zilizoendelea watu Wanaofanya mambo makubwa kwenye Jamii yanayotatua Changamoto huaminiwa na Taifa katika Changamoto za Kitaifa Marais wa Marekani kijamii ni wafanyabiashara wengine hata Silaha kuwa Amiri Jeshi Mkuu haiangalii interest za biashara zao za Silaha au viwanda na wengine walio na biashara nyingine bali uwezo wao na Serikali ni mfumo huamui peke yake tuondoe mashaka, hofu.
MAMBO SABA FURSA KWA WATEULIWA KUWEKA HISTORIA NJEMA Mambo haya yametokana na mijadala iliyokuwa inaendelea Mhe Waziri, Mkurugenzi na Bodi wakiyazingatia wanaowakosoa ndio watakuja kuwasifu
1.Watanzania wamesema wanataka kuona umeme wa elfu ishirini na saba (27,000) unaendelea na zaidi sana ukilipia ufungiwa kwa wakati
_ Jambo hili Waziri wa Nishati Mhe January Makamba, Mkurugenzi na Bodi hebu wekeni hata mfumo mtu akilipia mfumo uonyeshe kwa ngazi zote na Mamlaka ya juu na hata nchi nzima mtu akitaka kuangalia aone na hata idadi na orodha kwa ngazi ya Mikoa au Wilaya na hata Kata waliolipia ionekane tena kwa Umma na mtu akishafungiwa umeme mfumo uonyeshe ili mtu akilipia ombi likachukua muda mrefu mfumo uonyeshe. Watendaji wanaosimamia wawe wa ngazi zote wawe na uwezo wa kuuliza why Kuna wengi wamelipia hawajafungiwa?? na ndani ya TANESCO Mikoa au Wilaya za TANESCO wanaowafungia wateja haraka wapongezwe kwa kazi njema ya kuwafikia wateja.
Kifungiwa Umeme wa elfu ishirini na saba ni ndoto ya Mhe Rais kutatua adha ya gharama kubwa ili wananchi kuhimili.
Mhe Waziri, Mtendaji Mkuu na Bodi jambo hili hebu liwekeeni mikakati ya kulifanikisha zaidi ili Watanzania katika hili tuwe na kauli thabiti.
2.Watanzania wametaka Umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ukamilike kwa Kasi Serikali ya awamu ya Sita imeahidi hata kupitia Bunge itawezekana mapema Bwawa kuanza kufanya kazi ili kuzalisha umeme wa Gharama nafuu na wa Uhakika 2100 Megawati ili Malengo ya Nchi kuweza kuzalisha umeme wa Maji wa Gharama nafuu usiozidi Tsh 50 kwa unit liwezekane na zaidi kutumika kuendeshea miradi kama ule wa treni za umeme wa SGR kurejesha Fedha zilizotumika kwa Ujenzi wa Bwawa, Mradi wa SRG na zaidi kuweza kupunguza gharama za umeme na hata kuiwezesha TANESCO kujiendesha kwa kuwa mradi wa BWAWA ni fedha za ndani.
3.Watanzania hawataki mgao wa umeme ili kutoadhiri huduma za serikali na biashara za watanzania.
Mgao wowote wa umeme unaleta adha na Maneno mengi mengi kasi imepungua sana ya mgao tunaomba wakati huu usiwepo. Kila penye nia Pana njia.
4.Watanzania wanataka Kasi ya kurekebisha miundo mbinu ya Shirika la Umeme nchini iendelee hasa uwekaji wa nguzo imara za cement nguzo Bora na za gharama nafuu.
5.Vijiji elfu tatu (3000) nchini vilivyosalia kati ya elfu kumi na mbili (12,000) kufikiwa na umeme katika mradi wa REA. Mhe Waziri kazi kwako na Watendaji.
6. Huduma kwa wateja kwa changamoto za mtu mmoja mmoja kuhusu changamoto za umeme ziendelee kutiliwa mkazo katika utendaji wa kila siku.
7.Kodi ya Nyumba kupitia Luku ya Umeme Shirika liendelee kuwatambua wasio wamiliki.
Hivyo itoshe kusema Umekuwa mjadala mpana kutokana na mchango wa sekta ya Umeme nchini katika kutoa huduma, kuendesha maisha na shughuli za Uchumi kufanikiwa kwa Wizara ya Nishati ni kufanikiwa kwa Wizara nyingine na zaidi sana Watanzania wote na hata mmoja mmoja.
Na.
MwL. Cleopa E. Soi
NDOTO KUBWA
Masijala
0 Comments