Waandamanaji wakiwasha matairi moto kuziba barabara huko Khartoum, Sudan
Makumi kwa maelfu ya watu walikusanyika katika uwanja mkuu wa mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa kuonyesha kuunga mkono makabiliano baina ya serikali na muungano wa vikosi vya waasi kaskazini mwa nchi hiyo.
Mamlaka zilipanga maandamano haya ya Jumapili huku vikosi vya waasi vikiendelea kupiga hatua na shinikizo la kimataifa likiongezeka kutafuta suluhu la amani kwa vita vya mwaka mzima.
Baada ya kuteka miji muhimu ya kimkakati ya Dessie na Kombolcha katika eneo jirani la Amhara- takriban kilomita 300 kaskazini mwa Addis Ababa.
Waasi wa Tigray wanaonekana kufikiria kushambulia mji mkuu. Mikutano kama hiyo ilifanyika katika miji mingine kadhaa katika siku chache zilizopita.
Waandamanaji wameshikilia mabango yanayoonyesha kuunga mkono juhudi za vita za serikali. Hivi karibuni mamlaka imetoa wito kwa raia kusajili silaha zao za kibinafsi na kujiandaa kutetea nchi.
Nchini Sudan, vikosi vya usalama vya nchi hiyo vimewarushia mabomu ya machozi makumi ya walimu waliokuwa wakishiriki maandamano ya kuunga mkono demokrasia katika mji mkuu, Khartoum.
Kuna ripoti kwamba walimu wengi walikamatwa na vyombo vya usalama.
Waandamanaji walioandamana usiku kucha waliweka vizuizi kwa siku ya kwanza kati ya mbili za uasi uliopangwa wa raia kupinga mapinduzi ya mwezi uliopita.
Wanaitaka serikali ya kijeshi irudi nyuma na kuruhusu mabadiliko ya amani kwa utawala wa kiraia.
Maandamano hayo yanafanyika wakati wapatanishi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu wakiwasili Khartoum kwa mazungumzo ya kujaribu kutatua mgogoro huo.
Waziri Mkuu wa kiraia, Abdalla Hamdok, bado yuko chini ya kizuizi cha nyumbani na anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa wanajeshi kushirikiana nao, mwandishi wa BBC Andrew Harding anaripoti kutoka mji mkuu.
Kuna hofu kubwa ya kiusalama katika nchi hizi mbili, huku Jumuia za kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Marekani zikifuatilia kwa karibu mizozo inayoendelea, huku wito ukitolewa wa kurejeshwa kwa serikali ya kiraia Sudan na kumalizwa kwa mapigano Tigray, Ethiopia:Chanzo BBC
0 Comments