Mbwa waliofungiwa kwa ajili ya kuchinjwa huko Korea
Kulingana na Wakfu wa mbwa wa Korea Kusini bado njia ni ndefu katika kupata marufuku ya kudumu ya ulaji wa kitoweo cha nyama ya mbwa nchini humo.
Korea Kusini, Korea Kaskazini, China na Vietnam ni baadhi ya nchi ambazo bado zina tabia ya kufuga mbwa kwa ajili ya kitoweo cha nyama.
Katika mkutano na Waziri mkuu Septemba 27, Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in alisema kwa mara ya kwanza kwamba, " muda umefika wa kufikiria kwa umakini uwezekano wa kupiga marufuku ulaji wa nyama ya mbwa?" .
Bw. Moon Jae-in binafsi anafahamika kwa kupenda sana nyama ya mbwa. Ana mbwa kadhaa katika makazi yake yanayofahamika kama Blue House na alimuasili mbwa kwa jina Tory, aliyemchukua mwaka 2017 alipoingia madarakani.
Rais Moon Jae-in alimnusuru mbwa Tory kutoka shirika linalowanusuru mbwa la CARE mwaka 2017
Kwa mujibu wa takwimu za taasisi ya kimataifa ya Human Society za Septemba 2021, karibu mbwa milioni 2 hufugwa kwa ajili ya kitoweo cha nyama kila mwaka katika maelfu ya mashamba nchini Korea Kusini.
Sheria ya kulinda wanyama nchini humo huzuia tu mauaji ya kikatili ya mbwa na paka, lakini haizuwii ulaji wa nyama ya mbwa.
Serikali ya Korea Kusini pia imetumia sheria hii na sheria za udhibiti wa usalama wa chakula kumaliza mazizi ya mbwa kwa ajili ya nyama na migahawa inayouza nyama ya mbwa kabla ya matukio makubwa ya kimataifa kama vile Olympiki 2018 Pyeongchang.
'Rais aligusia tu marufuku ya ulaji wa nyama ya mbwa alipokuwa anakaribia kuondoka madarakani '
Rais wa Korea Kusini Moon Jae- wakati wa mkutano katika bunge la taifa Oktoba 25
Kulingana na Giny Woo, ukweli ni kwamba rais aliyeko mamlakani wa Korea Kusini kupiga marufuku ulaji wa nyama ya mbwa ni hatua muhimu.
Uamuzi ambao alisema kuwa ulikuwa ni matokeo ya miongo kadhaa ya kampeni ya wanaharakati wa wnyama na "ingepaswa kutangazwa mapema na Rais Moon Jae-in".
'Wakorea wengi wamegawanyika kuhusu suala la kula nyama ya mbwa'
Wizara za Korea bado hazijachukua hatua za kudumu za kuzuwia ulaji wa nyama ya mbwa
Tarehe 16 Oktoba, shirika la habari la Korea lilichapisha matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi inayopigia debe uelewa wa maslahi ya wanyama kuhusu maoni watu juu ya marufuku ya kudumu ya ulaji wa nyama ya mbwa.
Kulingana na utafiti huo, kati ya watu 10 walioulizwa kuhusu marufuku hiyo, watu 8 waliunga mkono kuzuiwa kuliwa kwa nyama ya mbwa na paka. Asilimia 48.9% waliunga mkono marufuku ya nyama ya mbwa na paka , asilimia 29.2% hawakukataa wala kukuunga mkono, 12.7% walipinga ulaji wa mbwa, kati yao asilimia 9.3% walionyesha upinzani mkubwa zaidi wa marufuku hiyo.
Katika mahojiano na BBC idhaa ya Vietnam, Bi Giny Woo alisema kuwa ingawa mtizamo wa watu kuhusu ulaji wa nyama ya mbwa unabadilika taratibu, wengi wao bado "wanatofautiana sana" na marufuku hiyo, kutokana na kwamba wamekua katika nchi inayofuga mbwa wa kuua na kupata nyama.
Ingawa mauaji ya kikatili ya mbwa yamekuwa yakionyeshwa kwenye Televisheni za nchi hiyo, vituo vya habari na mitandao ya kijamii kwa miaka mingi, bado safari ni ndefu katika kubadili mitazamo ya watu wa Korea Kusini kuhusu ulaji wa nyama ya mbwa.
Kulingana na Giny Woo, serikali iko kimya na umma umegawanyika kuhusiana na masuala ya maadili ya kuwauwa mbwa , "mbwa wataendelea kuuawa kikatili kwa ajili ya kuwala."
Madai ya Sheria ya kupiga marufuku ulaji wa nyama ya mbwa
Kulingana na Giny Woo, njia yenye ufanisi zaidi ya kuweka marufuku ya ulaji wa nyama ya mbwa ni kwa kupitia sheria.
"Kwa sasa, kampeni za kususia ulaji wa nyama ya mbwa zinazofanyika zikilenga mashirika na makampuni ya wenye magari ya utalii haviwezi kusaidia, lakini tunaamini ilikuwa na athari katika mapato ya mauzo ya nje.," alisema Giny Woo.
Kufanya hivi, katika Vietnam, ni muhimu sana katika kuiwekea shinikizo serikali ili ichukue hatua juu ya suala hili, kushirikiana kwa pamoja kufanya kampeni kutoka ndani na nje ya nchi, wanasema wanaharakati wanaopinga ulaji wa mbwa.
Katika nchi ya Vietnam, mamilioni yam bwa bado wanauawa kwa ajili ya kitoweo cha nyama. Uchinjaji wa mbwa na mauzo ya nyama yake umeshamiri na mbwa huchinjwa bila kupimwa, jambo linalosababisha hatari ya magonjwa ya kichaa cha mbwa. Je Vietnam itakuwa na marufuku ya kudumu ya ulaji wa nyama ya mbwa?...ni jambo la kusubiri kuona:CHANZO BBC
0 Comments