Header Ads Widget

HAKIELIMU YATOA RAI KWA SERIKALI

 



Licha ya kutolewa waraka wa elimu naomba 2 wa mwaka 2021 unaotoa maelekezo ya kumruhusu mtoto wa kike kurudi shuleni, Asasi ya Kiraiya isiyo ya Kibiashara (HakiElimu) wameiomba Serikali kujumuisha vipengele inavyotoa fursa ya watoto wa kike kurudi katika mfumo rasmi....Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo hii Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu,  Dr John Kalage ,amesema kuwa, waraka huo haujitoshelezi katika vipengele vya hatua gani zichukuliwe Ili mtoto arudi shuleni bila kubagulia, akijiamini pamoja na kulinda haki ya mtoto mtoto aliyezaliwa.


Aidha, amesema  kuwa, wameipomgeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuruhusu wanafunzi waliokatiza masomo kwa sababu ya kupata ujauzito kurejea masomoni kupitia mfumo rasmi, kupitia taarifa iliyotolewa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako.


"Pamoja na pongezi hizi, HakiElimu tunatoa Wito kwa Serikali sasa kukazia tamko na azma yake kwa kuhihuisha miongozo maalum inayomwezesha mtoto wa kike kurudi shuleni baada ya kujifungua ambao uliandaliwa lakini haukusainiwa kutokana na msimamo wa Serikali iliyopita"amesema Dr Kalage.


Ameongeza kuwa"Kwa mujibu wa tamko la Waziri Prof Joyce Ndalichako na baadae kufuatiwa na waraka rasmi uliotolewa na Serikali, kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania bara watoto walioacha shule kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata ujauzito, watarudishwa shule na kuendelea na masomo katika mfumo rasmi"amesema Dr  Kalage.


Amesema kuwa, ni vyema miongozo ikaandaliwa na kuanza kutumika mapema Ili kutoa fursa ya wanafunzi wa kike walioacha shule katika kati ya mwaka 2019 na 2002 aweze kurudi shule rasmi  kuanzia mwaka wa masomo 2022.


 Hata hivyo, amesema Kwa mujibu wa takwimu za Elimu (BEST 2020),mwaka 2015 wanafunzi wa kike 3,439 waliacha shule kwa sababu ya ujauzito, ambapo idadi imezidi kuongezeka hadi kufikia wanafunzi 6,533 mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la asimilia  90.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI