Header Ads Widget

CWT KITENGO CHA WANAWAKE WILAYA YA KIBAHA WAANDAA TAMASHA

 


CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT) kitengo cha Wanawake Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani kimeandaa tamasha la michezo litakalowashirikisha wanachama wanawake litafanyika Novemba 27 mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Kibaha katibu wa CWT kitengo cha Wanawake Wilaya ya Kibaha na mwenyekiti wa soka la wanawake mkoa wa Pwani Florence Ambonisye alisema kuwa tamasha hilo litafanyika kwenye uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC).


Ambonisye alisema kuwa baadhi ya michezo itakayoshirikishwa ni pamoja Rede, riadha, kukimbia na yai, netiboli na kutunga uzi ambapo zawadi ni pamoja na  soda,vitenge na tisheti na mgeni rasmi atakuwa mweka hazina wa CWT Taifa Abubakari Allawi.


"Dhumuni la tamasha hili ni kujena Umoja na ushirikiano baina ya walimu pia kuwasajili ili wawe wanachama na kuboresha afya na kuwahamasisha washiriki michezo,"alisema Ambonisye.


 Alisema kuwa wataanzisha timu ya netiboli ya wanwake ambapo kwa wanaume wana timu ya soka ya CWT ya Wilaya ya Kibaha hivyo nao wataanzisha ili ishiriki mashindano mbalimbali ya kitaifa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI