Header Ads Widget

EU, UWABA WATUMIA BAISKELI KUHAMASISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA




UMOJA wa Ulaya (EU) hapa Nchini kwa kushirikiana na Umma wa Wapanda Baiskeli Dar es Salaam [UWABA], mapema leo 28 Novemba wameandaa na kushiriki matembezi ya baiskeli ya umbali wa KM 10 (msafara wa baiskeli) wakiongozwa na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Suleiman Jafo (MB) matembezi hayo yenye kauli mbiu "Tunza Mazingira,  Tumia Baiskeli.".......NA Andrew Chale


Katika matembezi hayo, wapanda Baiskeli zaidi ya 200 walishiriki wakiwemo watoto wadogo umri wa kuanzia 12,wandesha baiskeli walemavu pamoja na wananchi mbalimbali waliokuwa na baiskeli binafsi walipata nafasi ya kuungana kila walipopita wapanda baiskeli hao.



Awali akizungumza katika tukio hilo mara baada ya kuhitimisha matembezi ya KM 10, ya Baiskeli, Balozi wa EU, Mhe. Manfredo Fanti alipongeza wananchi wa Dar es Salaam kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo licha ya uwepo wa mvua kubwa ambapo pia ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri Jafo kuendelea kupambania Watanzania kwenye masuala ya mazingira.


Aidha, alisema kuwa licha ya utaratibu wa uendeshaji na upandaji  baiskeli ni wa muda mrefu, umekuwa ukisaidia  utunzaji wa mazingira  na kuweka mazingira rafiki.


"Hii ni fursa ya kipekee kwa Umoja wa Ulaya kushirikiana na UWABA kwa pamoja kuwezesha wapanda baiskeli na kufanikisha tukio hili muhimu.



Sote kwa pamoja tufahamu kuwa tunahitaji kubadilisha mifumo yetu ya maisha ikiwemo usafiri tunaotumia zaidi tuwe makini zaidi. Wapanda baiskeli wao wanatumia kunyonga baiskeli wakiimalisha afya na kuweka mwili salama." Alisema Balozi wa EU , Mhe. Manfredo Fanti.


Kwa upande wake Mgeni rasmi katika tukio hilo, Waziri, Mhe. Suleiman Jafo amepongeza  Umoja wa Ulaya pamoja na UWABA kwa kuendelea kupigania uhai wa mazingira hususani katika matumizi ya baiskeli ambapo watumiaji wake wamekuwa wakiunga kampeni kwa vitendo utunzaji wa mazingira.


"Leo ni siku ya baraka sana, sababu tunajenga ajenda ya kupanda miti, tumeweza kupata mvua na tumeanza nayo na tumekuja kumaliza nayo wakati wa matembezi yetu haya ya baiskeli.



Jambo hili linaunga kampeni kabambe ya kimazingira ndani ya Tanzania, ambayo ni kauli kubwa ya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan, siku ya leo wakati tupo kwenye mbio za baiskeli na ajenda ya kupanda miti, kutunza mazingira, Mungu ameleta mvua  kubwa sana hii ni baraka zake kubwa sana."


Waziri Jafo aliongeza kuwa, Tanzania na Nchi zingine hali imekuwa mbaya ikiwemo ongezeko la joto kama Mataifa  mengine wanavyolalamikia hali hiyo kutokana na mabadiriko ya tabia nchi.


 "Makundi haya niliyoyaona hapa ikiwemo watoto, wanawake, wazee na mabalozi walioshiriki matembezi haya ya baiskeli kwakweli yamenifariji sana, binafsi naona Tanzania ile inayosonga mbele kwenye mazingira." alisema Waziri Jafo.



Waziri Jafo aliongeza kuwa, wamepata taarifa ya kuwa "mbuzi na ng'ombe wanakufa kutokana na ukame, pia upande wa maji kama visiwa baadhi vimeanza kukauka na vipo hatarini kutokweka, hivyo kupitia matembezi hayo ya baiskeli utachochea utunzaji wa mazingira na kuzuia athari zaidi." Alimalizia Waziri Jafo.


Nae Mweyekiti wa UWABA, Bw. Meja Mbuya akizungumza kwa niaba ya Umma wa wapanda baiskeli, aliwashukuru Umoja wa Ulaya kwa kuendelea kuunga mkono na kutambua wapanda baiskeli kwani ni mabalozi endelevu kwenye masuala ya mazingira.



"Huu ni mwaka wa 18 tangu kuanzishwa kwa tukio hili na tumendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya kila mwaka na kila shughuli zinazohusiana na mazingira. Nawaomba wadau tunendelee kujitokeza kwa wingi kushiriki matembezi ya baiskeli kwani zinafaida nyingi  ikiwemo kulinda afya ya mwili, lakini pia kulinda mazingira yetu." alisema Meja Mbuya.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI