Header Ads Widget

WAZAZI WAASWA KUTOWAGOMBEZA WATOTO

 



 Wazazi Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuwa karibu na watoto  wao hususani katika kuwasikiliza kwani kwa kufanya hivyo watoto wanakuwa huru kueleza Yale ambayo wanakumbana nayo .Na Rehema Abraham, Kilimanjaro


Amesema hayo Sarafina Labani wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la watoto lililofanyika katika viwanja vya shule Ya Diomed  Excellence Academy   Iliyopo njia panda ya Kcmc mkoani Kilimanjaro.


Aidha amesema watoto hawapaswi kugombezwa Bali wanatakiwa wasikilizwe ili  waweze   kueleza  kwa uwazi Yale Mambo ambayo wamekutana nayo katika jamii.


"Kama tunavyojua watoto wanapitia Mambo mengi ya ukatili wa kijinsia ,lakini mzazi Kama utampa mtoto nafasi ya kumsikuliza ,kimuelewa na kumkagua mara kwa mara anapotoka shuleni utapata kutambua matatizo anayomkumba nayo na hii itasaidia kupunguza matatizo  ya ukatili wa kijinsia"Alisema Sarafina.


Katika hatua nyingine ameishauri Serikali kuangalia ni namna gani inaweza kufanya ili vipaji vya watoto viweze kuibuliwa kwani vipaji ni Ajira na vinaweza kuwasaidia katika maisha Yao ya baadae .



Kwa upande wake muandaaji wa tamasha hilo Diomed Paskal Amesema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuibua vipaji vya watoto ili waweze kuwaendeleza na viweze kuwasaidia kwa maisha ya baadae .


Amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya watoto wanaolelewa na wasichana ,kwani watoto hao wamekuwa wakijifunza vitu vibaya hivyo ni vyema wazazi wakapeleka watoto wao katika vituo ambako Kuna usalama wa kutosha.



Hata hivyo watoto walioshiriki katika tamasha hilo wamewaomba   kuwaendeleza watoto wao ambao Wana vipaji ili viweze kuonekana na kutambulika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI