Header Ads Widget

CHODAWU WAIOMBA SERIKALI KURIDHIA MKATABA NAMBA 189 WA KAZI ZA NDANI KWA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI



CHAMA cha wafanyakazi wa Majumbani Hifadhi ,mahotelini, huduma za jamii na ushauri CHODAWU wanaiomba serikali kuridhia mkataba namba189 wa kazi za ndani kwa wafanyakazi wa majumbani....Na Mwandishi wetu Hamida Ramadhan Dodoma 


Akiongea leo na kituo hiki mkuu wa Idara ya Sheria CHODAWU Asteria Gerald amesema mkataba huo ulipitishwa Nchini Jeniva mwaka 2011 na nchi wanachama wote walipaswa kulidhia mkataba huo sasa ni kipindi kirefu Nchi ya Tanzania bado haijaridhia mkataba huo kama serikali haijaridhia hawezi kuwa sheria. 



Bila ushawishi bila kutoa elimu ya kutosha serikali haitaweza kutambua na kuelewa ni kitu gani kipo ndani ya mkataba huo namba 189 na ndio maana  tunapambana serikali yetu ili iweze kuridhia iwe sheria iweze kuwalinda wafanyakazi wa ndani waliosahaulika kwa kipindi cha muda mrefu kwani watu hawa wamejiweka kama vile sio wafanyakazi wa ndani wakati ni wafanyakazi kama wengine.


Amesema sheria tulionayo mpaka sasa hivi ya ajira ni sheria pana haisema mfanyakazi huyo anatakiwa hivi na huyu anatakiwa kupata haki hii imeongelea wafanyakazi wote lakini kungekuwa na sheria au kifungu ingekuwa rahisi kumtetea mfanyakazi wa majumbani.


Matarajio yetu baada ya serikali kuridhia wafanyakazi wa majumbani wanatakiwa kuangaliwa kwa jicho pana na utetezi wao kwa ajili ya  maslahi yao ili  kulindwa na sheria hiyo.



Kwa upande wake Mratibu wa Mradi CHODAWU Deograsia Vuluwa amesema lengo la semina hiyo ni kuona kikosi kazi chenye lengo ya kuridhia mkataba wa 189 kinakutana pamoja na kuona nini cha kufanya kwa hatua ya baadae .


Amesema chama hicho kinajivunia kuona angalau sasa wafanyakazi wa ndani wanatambua haki zao ambapo amesema sasa mfanyakazi wa ndani anaweza kupata haki zake za msingi kupitia CHODAWU.


Naye mfanyakazi wa majumbani Jenipha Sudai ameiomba seriklai kulidhia mkataba huo ili ikawe neema kwao kwani wameteseka kwa kipindi cha muda mrefu .


" Mkataba huu ukiridhiwa na serikali  na sisi wafanyakazi wa majumbani tutakuwa na kinga hata pale tunapodhulumiwa haki zetu sheria itakuwepo na kututetea,"amesema 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI