Header Ads Widget

BONYOKWA YAANZA UTEKELEZAJI PESA ZA UVIKO 19, YAMPA TANO RAIS SAMIA

 



Na Fatma Ally, MDTV Dar es Salaam


Halmashauri za mkoa wa Dar es Salaam zimeanza utekelezaji wa Mradi wa Shule ya Sekondari Bonyokwa ambapo madarasa 12 yanatarajiwa kujengwa kwa lengo la kuondoa upungufu wa vyumba vya madarasa katika Kata hiyo.


Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa, Shaaban Maliyatabu amesema kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kutakwenda kupunguza changamoto ya wanafunzi kukaa chumba kimoja wengi.



"Tunamshukuru na kumpongeza  Rais wa JMT Samia Suluhu Hassan kwa zawadi  ya madarasa 12 aliyotupatia pesa kutoka uviko 19 hii imekua zawadi bora ya kufunga na kufungua mwaka kwa watoto wetu kupata mahala bora na Salama pa kujifunzia"amesema Maliyatabu



Ameongeza kuwa,  Rais wa JMT Samia Suluhu Hassan amefanya  kazi kubwa katika kuleta maendeleo kwa kugusa maeneo muhimu yote ikiwemo kwenye Miundombinu ambapo mradi huo unategemewa kukamilika kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na fedha za kukamilisha mradi huo zipo, kwa  wakati.



"Hakuna kitakacho sababisha ujenzi huu kukwama kwani pesa zipo za kutosha, Rais Samia amefanya kazi kubwa anastahili kupongezwa kila kona kwa lengo la kumtia moyo, tunakwenda kujenga vyumba madarasa 12 ambapo ujenzi wake utagarimu sh mill 240" amesema Maliyatabu.


Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bonyokwa, Upendo Mgaza amesema kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutapunguza idadi kubwa ya wanafunzi  kukaa katika darasa moja ambapo changamoto hiyo ilikua ya muda mrefu.



"Tunaishukuru sana Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutujengea madarasa haya kwa sasa wanafunzi wetu wataweza kukaa chumba kimoja wanafunzi 56, tofauti na mwanzo walikvyokua wanakaa wengi katika chumba kimoja"amesema Mgaza

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI