Waziri wa sanaa na michezo Innocent Bashungwa anatarajiwa kufungua maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukizwa yatayofanyika kitaifa mkoani Arusha mnamo Novemba 6 mwaka huu. mwandishi wa matukio daima Teddy Kilanga anaripoti kutokea Arusha
Akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho hayo, Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella alisema kuwa kumekuwa na juhudi kubwa za kuzuia na kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo pia Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu amekua akishiriki kupambana nayo kuanzia akiwa makamu wa Rais na hata sasa.
Aidha alisema magonjwa hayo ni moyo, shinikizo la juu la damu, Pumu, afya ya akili na ajali, ikiwa takwimu za kidunia zinaonyesha kuwa mpaka sasa magonjwa hayo yanachangia zaidi ya asilimia 71 ya vifo, takribani watu milioni 57 kwa takwimu za mwaka 2016.
Mongella alisema nchi ya Tanzania asilimia 33 ya vifo vinasababishwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza hadi mwaka 2020 watu milioni 4.7 wamepoteza maisha kwa magonjwa hayo ambapo aliongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan katika awamu ya sita amekuwa akiweka juhudi nyingi sana kwa ajili ya kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa hayo.
"Juhudi hizo tumeona hivi karibuni ikiwemo ujenzi wa ICU 272,x -ray 85,Stiscan 29 ikiwa mwisho wa siku miundombinu yote itapelekea katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwenye kusaidia afya na tiba ikiwa kuanzia Novemba 6 hadi 13 maadhimisho hayo yatafanyikia mkoani Arusha,"alisema Mongella.
Watakaoshiriki katika maadhimisho hayo ni pamoja na waziri wa elimu Joyce Ndalichako na Waziri wa Tamisemi,Ummy Mwalimu na yatafungwa na waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Dkt.Doroth Gwajima mnamo Novemba 13 mwaka huu
0 Comments