Header Ads Widget

WANAFUNZI MKOANI KAGERA WAMESHAURIWA KUJIUNGA NA SKAUTI.

Vijana walioko mashuleni katika mkoani Kagera wameshauriwa kujiunga na skauti kwani itawasaidia kupata stadi za maisha. mwandishi wa matukio daima Titus Mwombeki anaripoti kutokea Kagera

Hayo yalisemwa na  Katibu Tawala wa mkoa wa Kagera Faustine Kamuzola akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Kagera ambaye ni mlezi wa skauti wa mkoa huo Meja Jenerali Charles Mbuge wakati wa makabidhiano ya mwongozo wa mafunzo kwa waelimishaji kufundisha vijana wa skauti ambapo alisema kuwa skauti ni jeshi kubwa na taifa linawategemea sana  na sio kwa kupambana na rushwa tu hata kupambana na majanga mbalimbali yanapotokea.

“ Skauti ni jeshi kubwa tunawategemea sana lakini pia nje na skauti kuwafundisha vijana uzalendo skauti pia usaidia vijana kupata stadi za maisha, mimi binafsi niwaombe walimu pamoja na viongozi wa skauti mlioko hapa muwaimize vijana walioko mashuleni wajiunge na skauti kwani itawasaidia kupata stadi mbalimbali za maisha nje na elimu ya kwenye vitabu” alisema

Kwa upande wake Afisa Elimu mkoa wa Kagera Khalifa Shemahonge alisema kuwa kupitia skauti kwa kushirikiana na TAKUKURU ni umoja ulioundwa  kutokana na nguvu waliyonayo skauti na kuongeza kuwa mwongozo huo uliokabidhiwa leo utapelekwa kwa wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri, maafisa elimu na hatimaye kwenda kwa vijana wote kwani rushwa ni ni moja ya matukio mabaya yanayopelekea  kurudisha Maendeleo ya nchi nyuma.

“Mafunzo haya yanapendeza sana ukiwapitia vijana hasa vijana wadogo ambao wapo mashuleni na mimi naamini kupitia  mwongozo huu utasaidia sana katika mapambano dhidi ya rushwa” alisema Shemahonge

Naye John Joseph Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa kagera alisema kuwa  wao kama TAKUKURU moja ya kazi zao ni  kushirikiana na makundi mbalimbali katika kuhakikisha yanatoa elimu juu ya madhara ya rushwa, na skauti ni kundi lenye nguvu sana tunaamini watakuwa mabalozi wetu wazuri katika kutoa elimu hiyo.

“Skauti ni kundi lenye nguvu kwani linashirikisha vijana wengi walioko mashuleni katika kulinda amani na kutoa elimu juu ya mambo mbalimbali na sisi kama TAKUKURU mkoani Kagera tumeamua kushirikiana na skauti katika kuelimisha vijana wenzao juu ya mapambano  dhidi  ya rushwa kwa kutumia   mwongozo uliozinduliwa leo”. alisema

Akisoma risala ya skauti mbele ya Katibu Tawala wa mkoa huo Shalone Respikius mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Mafumbo iliyoko Manispaa ya Bukoba alisema kuwa moja ya lengo la kukabidhi mwongozo huo ni kumfanya mlezi wa skauti Mkoani humo  kuufahamu mwongozo huo utakaotumika kuelimisha wawezeshaji watakaoshiriki katika kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa Kwa vijana wa skauti na vijana wengine.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI