Mapendekezo hayo yametolewa mara baada ya kuwa na Changamoto za Kudumu katika kuhifadhi na Kulinda Rasilimali zisizorejesheka visiwani hapa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,Nishati na Madini Zanzibar Dkt Mngereza Mzee Miraji Amesema kuwa, Wizara imeandaa mikakati mbalimbali ya kiutendaji katika kudhibiti rasiliamali za Nchi.
“Moja ya mkakati ni kuandaa kikao hichi ambacho kilikuwa na lengo kuona hatua mbalimbali za kiutendaji ambazo Wizara imekuwa ikichukua na hatua ambazo zinakwenda kuchukua katika kuhifadhi rasilimali na kuongeza Mapato,”alisema.
Alisema kuwa kutokana na Kikao hicho kumeonekana kuna umuhimu wa kuweka nguvu za pamoja kwa Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali kuhusishwa katika kudhibiti Mapato yatokanayo na Rasilimali zisizorejesheka.
“Sote kwa pamoja tumeona kama kuna umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja ili kulinda hizi rasilimali zetu pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali,”aliongeza
Hata hivyo Dkt Mngereza alieleza kwamba, kumekuwa na Changamoto ya Taarifa kwa Taasisi za Serikali katika kuzuia uchimbaji wa Mchanga, Mawe na vifusi na kupelekea athari ya kimazingira na kupoteza Mapato.
Alieleza kuwa Wizara sasa imejipanga kuondoa Changamoto zote zinazowakabili katika kulinda na kuhifadhi Maliasili zote zisizorejesheka.
Hatua nyingine aliwahakikishia wajumbe wa kikao hicho kuwa katika kipindi cha uongozi wake katika Wizara hiyo atahakikisha kila Wananchi wanapata huduma zilizobora.
Nao washiriki wa Mkutano huo wakiwemo Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali ndani wameeleza kuwa kuna changamoto nyingi katika kulinda rasilimali zisizorejesheka.
“Kuna Changamoto nyingi zikiwemo ushirikishwaji mdogo kwetu, Changamoto ya kuingiliana kiutendaji baina ya taasisi na taasisi,”Walieleza.
Kikao hicho cha Pamoja kimehusisha Wizara mbalimbali zenye usimamizi wa Mapato na Rasilimali, Wakuu wa Wilaya, Halmashauri, Mabaraza ya Manispaa, Mabaraza ya Miji pamoja na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa.
0 Comments