Header Ads Widget

Waziri wa Uhispania aapa kupiga marufuku ukahaba



Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez ameahidi  kupiga marufuku ukahaba nchin humo.

Akiongea na wafuasi mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa Chama chake cha Kisoshalisti huko Valencia, Bw Sanchez alisema kwamba kazi hiyo "inawatumikisha" wanawake.

Ukahaba ulihalalishwa nchini Uhispania mnamo 1995 na mnamo 2016 UN ilikadiria kuwa tasnia hiyo ilikuwa na thamani ya € 3.7bn (£ 3.1bn, $ 4.2bn) huku utafiti wa mwaka 2009 uligundulika kuwa hadi 1 kati ya wanaume 3 wa Uhispania walikuwa wamelipia ngono.

Walakini, ripoti nyingine iliyochapishwa mnamo 2009 ilipendekeza kwamba idadi hiyo inaweza kuwa juu kama 39% na utafiti wa UN wa 2011 ulitaja Uhispania kama kituo cha tatu kikubwa cha ukahaba ulimwenguni, nyuma ya Thailand na Puerto Rico.

Kazi hiyo nchini Uhispania haijathibitiwa kwa sasa, na hakuna adhabu kwa wale wanaotoa huduma za ngono zilizolipwa kwa hiari yao ilimradi haifanyiki katika maeneo ya umma. japokuwa  kufanya kazi ya uwakala kati ya kahaba na mteja sio halali

Sekta hiyo imeshamiri tangu kutolewa kwa marufuku ya ukahaba na inakadiriwa kuwa karibu wanawake 300,000 hufanya kazi kama makahaba nchini Uhispania.

Mnamo 2019, Chama cha Bwana Sanchez kilichapisha ahadi katika ilani yake ya uchaguzi ya kupiga marufuku ukahaba, kwa kile kilichoonekana kama hatua ya kuvutia wapiga kura zaidi wa kike, Ilani hiyo iliita ukahaba "moja ya mambo ya kikatili zaidi ya kuhimili umaskini na moja ya aina mbaya zaidi ya unyanyasaji dhidi ya wanawake".

Hata hivyo miaka miwili kuendelea kutoka kwa uchaguzi, bado hakuna sheria iliyowasilishwa.

Wafuasi wa mfumo wa sasa wa Uhispania wanasema kwamba imeleta faida kubwa kwa wanawake wanaofanya kazi katika biashara hiyo na kufanya maisha kuwa salama kwao.

Walakini katika miaka ya tangu uchaguzi wasiwasi mkubwa umeibuka kuhusu uwezekano wa wanawake kusafirishwa kwenda kufanya kazi hiyo bila hiari yao . Mnamo mwaka wa 2017, polisi wa Uhispania waligundua wanawake 13,000 katika misako ya kupambana na biashara ya ulanguzi wa watu wakisema kwamba angalau 80% yao walikuwa wakitumiwa dhidi ya mapenzi yao na mtu mwingine.

Chanzo; BBC Swahili

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI