NA JACOB SONYO, KYELA -MBEYA
Wakulima wa zao la mpunga wa skimu ya umwagiliaji kijiji Cha Ngana Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya wameshiriki zoezi la kupiga Kura ili kuchagua mbegu Bora ya zao hilo.
Wakizungumza na Kituo hiki baadhi ya wakulima hao wamesema licha ya kuwepo kwa wingi wa mbegu ya zao hilo lakini bado kumekua na chagomoto hasa katika soko kutokana na kukosa sifa za ziada .
Andrew Mwakipeta ni mmoja wa wakulima wa zao hilo anasema wataalam wamekua wakiwaletea mbegu bila ya kuwashirikisha jambo ambalo wamekua wakikumbana na changamoto ya soko licha ya kupata mavuno mengi kutokana na mbegu hizo kukosa sifa ikwemo ladha, kunukia na muonekano mbaya wa mchele
" mbegu zipo nyingi Sana lakin kila mbegu imekua na sifa yake ila inapokuja sokoni inakosa wateja jambo ambalo bado ni changamoto kwetu "amesema Abdalh
Taasisi ya utafiti wa Kilimo Nchini (TARI ) Dakawa kushirikiana na shirika la AATF kutoka nchini Kenya wanaendesha zoezi la kushirikisha wakulima Katika tafiti za mbegu bora ya zai Hilo ili watoe maoni yao wanahitaji mbegu yenye sifa ya aina gani itakayoweza kuwainua kiuchumi.
Barnabas Sitta ni afisa mtafiti wa TARI Dakawa anasema zoezi hilo litakua lenye mafanikio kwani licha ya Taasisi hiyo kuzalisha mbegu za aina tofauti ya zao la mpunga na zenye sifa Bora lakin bado zimekua na Changamoto ya mapokezi kwa wakulima .
"tumeona tushirikiane na wakulima Katika tafiti za mbegu tunazozalisha Ili kuondoa malalamiko ya wakulima madai ya kuletewa mbegu ambazo sio rafiki kwao kutokana na mazingira na hali ya hewa ya eneo husika" Barnabas Sita mtafiti TARI Dakawa
Kwa upande wake afisa mradi shirika la AATF kutoka nchini Kenya Millicent Sedi amesema lengo la mradi huo kuwanufaisha wakulima wa zao hilo Ili kujikomboa kiuchumi.
Sedi amesema wakulima wengi wa zao la mpunga Nchini Tanzania wamekua wakizalisha kwa wingi zao Hilo lakini wameshindwa kujikomboa kiuchumi hivyo tafiti hizi zitaleta tija kwao.
" Tunataka kuwabadili wakulima wa mpunga kutoka Kilimo Cha kizamani kulima Kilimo Cha kisasa hasa Katika uchaguzi wa mbegu Bora "amesema Millicent afisa mradi AATF
MWISHO





0 Comments