Header Ads Widget

WAVUVI TISA MKOANI KAGERA WANUSURIKA KIFO NDANI YA ZIWA VICTORIA.

Wavuvi wapatao tisa mkoani kagera wamenusurika  kifo baada ya kuvaniwa na watu ambao ni  maafisa wa jeshi la majini mkoani humo na kuwanyang'anya kwa nguvu vifaa pamoja na mafuta na kuacha mitumbwi yao ikielea majini mwishowe  kuokolewa na jeshi la majini la nchini Uganda.  mwandishi wa matukio daima Titus Mwombeki anaripoti kutokea Bukoba

Akizungumza kwa niaba ya wengine mmoja ya wavuvi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mzee  Steven mkazi wa Nyabesiga mkoani Kagera   katika mapokezi yao mbele ya mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na TAKUKURU katika bandari ya kastamu mkoani humo ameelezea kuwa walitelekezwa na jeshi la majini la mkoa wa Kagera na kuwanyanganya baadhi ya vifaa pamoja na mafuta na kuacha mtumbwi wao ukielea.

“Tukiwa majini tuliona boti ya jeshi la polisi wa majini ya hapa wakafika wanatuuliza mnatumia aina gani ya mitego na sisi tulijibu nchi sita ambayo inakubalika, askari mmoja akashuka kwenye boti akaja kwenye boti yetu kukagua alipoona nikweli akasema kateni nyavu kwanguvu baadaye wakachukua matenki ya mafuta na forline wakaweka kwenye boti yao wakaondoka na kutuacha tukielea na boti letu bila masaada wowote” alisema Steven

Ameongeza kwa kulishukuru jeshi la majini nchini Uganda na uongozi wa mkoa wa Kagera kwa msaada walioutoa kwao kwa kuhakikisha wao wanakuwa salama mpaka sasa.

Naye mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge alisema kuwa alipokea taarifa hizo kutoka kwa   baadhi ya wanahabari juu ya kupotea kwa watanzania wapatao tisa ndani ya ziwa Victoria na baada ya hapo hatua za ufuatiliaji zilianza kufanyika  ili kuweza kuwapatia wavuvi hao. 

“Nilipata taarifa ya janga hili tarehe 12/10/2021 usiku kwamba kuna wavuvi tisa watelekezwa ziwani baada ya kunyang’anywa matenki ya mafuta na baada ya hapo nilimuita afisa anayesimamia masuala ya uvuvi katika mkoa wetu na watendaji wengine wa mkoa, na mpaka sasa mtuhumiwa mmoja ambaye ni afisa uvuvi mkoani Kagera anashikiliwa kwa ajiri ya uchunguzi wa tukio hili”. alisema Jenerali Mbunge

Aidha, Mkuu wa mkoa huo amekemea vikali watumishi  wa umma wenye tabia za kuwaonea watanzania na kusema kuwa sheria kali zitachulia dhidi ya kiongozi yeyote wa serikali atakayekiuka sheria na kuwanyanyasa wenzake.

Kwa uapande wake Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa kagera JOHN JOSEPH amesema tayari uchunguzi wa suala hilo upo katika hatua za mwisho na ukikamilika taarifa itatolewa.

“ Baada ya kupata taarifa hizi sisi kama TAKUKURU mkoani Kagera tulianza uchunguzi mara moja ili kubaini ukweli wa jambo hili na tayari suala hili lipo hatua za mwisho lilikamilika taarifa zitatolewa” Kamanda Joseph.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI