Na Mwandishi wetu, MDTV Kigoma
Wakulima wa zao la chikichi mkoani Kigoma wamepatiwa mafunzo ya jinsi ya kuandaa mashamba na kulima zao hilo kwa mbegu mpya ya Tenera.
Akizungumza mara baada ya kupata mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari Nassoro Juma mkulima wa zao Michiki alisema kuwa ameridhika na mafunzo hayo.
Alisema kuwa mafunzo haya yata ongeza ujuzi namna bora ya kuyaandaa na kuyatunza mashamba mapya ya chikichi.
"Hili zao lilikuwa halipewi nafasi kabisa lakini uwepo wa kituo cha Tari na hamasa ya serikali juu ya zao hili tumehamasika kulima tunachotaka kwa sasa ni mbegu tu" alisema Juma
Mkurugenzi Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania TARI Kihinga Dr. Filson Kagimbo anakuwa ametoa mafunzo hayo kwa Wakulima ili kuboresha zao hilo.
Alisema kuwa wakulima wengi hawakuwa na elimu juu ya namna bora ya kutunza michikichi ambapo utolewaji wa elimu hiyo kwa wakulima utasaidia kuboresha mashamba ya Chikichi.
"Unajua elimu ya zao la Chikichi ni mpya sio kwa wakulima tu hata kwa maafisa ugani ndio maana tunatoa elimu kwa wote ili waweze kushirikiana kusimamia na kuyaboresha"
“Unajua mkulima akishiriki mafunzo haya tunahakikisha kuwa anatoka akiwa anajua kila kitu kuanzia namna ya kuweka kwenye kiriba kidogo kisha kuhamishia kwenye kikubwa baadae kuandaa shamba na kufanikiwa kupanda" alisema Dr Kagimbo
0 Comments