Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Chama cha NCCR- MAGEUZI kupitia Kamati kuu ya chama hicho imesema hakitashiriki wala kuwa sehemu ya mkutano uliondaliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mtungi ambao unatarajia kufanyika Octoba 21 hadi 23 jijini Dodoma.
Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia amesema maamuzi hayo yametokana na kikao kilichokaliwa October 17 na wajumbe wa kamati hiyo kwa masala sita ambapo wamesema wamefikia uamuzi huo kwa nia njema.
"Sisi NCCR MAGEUZI katika kikao chetu cha jana kwa misingi ya Utu tulizungumzia ajenda moja ya mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa na kurejea ibara ya 26 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaeleza kuwa kila mtu anawajibu wa kufuata na kuitii katiba hiyo na Shughuli za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia kila mtu anahaki kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria ikiwemo kuchukua hatua za kisheria"amesema Mbatia.
Nakuongeza kuwa katika hiyo pia inaeleza kuwa haki ya kufanya mikutano sio ridhaa ya mtu bali ni haki ya msingi kwani uitaji kuomba fadhira kwa mtu kuhusu haki hizi"alisisitiza
Aidha, amesema hakuna sehemu yoyote ambayo Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi alivisihi vyama vya Siasa kusimamia katiba na kufuta sheria na kueleza kuwa pale anapoona katiba inavunjwa anapaswa kusimama na kueleza kuwa katiba inavunjwa bila kuogopa.
Akitolea mfano amesema Agusti 28 mwaka huu Kamati kuu ya chama hicho ilikutana na wajumbe katika hotel ya lamada kufanya mkutano wa ndani ambao ulivunjwa na Jeshi la Polisi nchini tulikuwa na jumuiko la watu 30 na kueleza kuwa baada ya tukio hilo awakusikia Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akisema lolote .
"Tunakumbuka Septemba 6 mwaka huu Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi alitoa hotuba yake kuwa anaomba makongamano, mikutano viache kufanyika mpaka mazungumzo yafanyike alitoa kauli hiyo"amesema Mbatia
Amesema kuwa, baada ya tamko hilo kuna baadhi ya vyama vya Siasa ikiwemo Chama Cha Mapinduzi CCM kiliitisha mikutano kikubwa katika kanda ya kusini na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi hakuweza kusema lolote .
Hata ivyo, amesema kwa sasa kinachofanyika ni ubaguzi ambao hauwezi kuvumilika na mtu yoyote pia ni dhihaka kwa vyama vya Siasa hususani NCCR MAGEUZI kwa kitendo walichofanyiwa.
Amesema kuwa, hatua iliyochukuliwa na Chama hicho kitajikita katika kukutana na wadau wa Demokrasia na vyama vingine ambavyo ni wahanga wa unyanyaswaji ili kupata suhulu ya pamoja ya kukabiliana na chagamoto hizo kwa maslahi ya mapana ya mama Tanzania.
Ameongeza kuwa, kutokana mambo yanavyokwenda kwa sasa, mwaliko kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa chama hicho hauna maslahi yoyote kwao.
Hata hivyo, amesema Chama hicho kinaamini kuwa utaratibu ukishawekwa katika jambo lolote usipofatwa unaweza kusababisha fujo, huku akieleza utaratibu uliokubaliwa ni wa kuongozwa na katiba kwani ndio sheria mama .
"Taifa hai linaongozwa na katiba hai hivyo upo umuhimu wa kuhakikisha katiba hii inafatwa Rais Samia Suluhu Hassan alivyokula kiapo Machi 19 mwaka huu alishika katiba ambayo inaelekeza haki ya kujumuika ni haki ya msingi ya kikatiba"amesema Mbatia.
Amesema kuwa,
kilichopaswa kufanyika ni kuwepo kwa kongamano la Amani ambalo lilifanyika katika Serikali ya awamu ya nne ambalo lilifanyika kwa ushirikishwaji mkubwa.
Ikumbukwe hivi karibu Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilitagaza kukutana na wadau mbalimbali wa vyama vya Siasa ikiwemo Jeshi la Polisi kwa lengo la kuweka majadiliano ya kuweka suhulu kati vyama vya Siasa na Jeshi hilo.
Msajili wa vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi alisema lengo la vikao hivyo ni kuweka mazingira rafiki na maelewano baina ya vyama Siasa.
0 Comments