Na Mwandishi wetu, Kigoma
Kufutia taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania tari kituo cha kihinga kuja na mbegu mpya ya chikichi aina ya tenera baadhi ya wakulima wa zao hilo wameanza kuitikia wito wa kukata miti ya zamani na kupanda miti mipya.
Awali wakulima wamekuwa na mashamba makubwa lakini hayana tija ujio wa tenera kwetu ni mkombozi tunaamini kuwa hamasa hii inayotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa itakuwa na manufaa makubwa kwetu.
Akizungumza shamabani kwake mara baada ya kutembelewa na watalaamu kutoka Tari Amri Juma kutoka kata ya kibirizi mkoani kigoma alisema kuwa ipo faida kubwa ambayo tunaweza kupata tena ikikuwa kwa muda muafaka na ikawa na matunzo mazuri itasaidia sana.
“Mimi niliamua kukata miti 100 ili niweze kupanda miti mipya shambani kwangu yaani niweke mbegu za kisasa ambazo ndani ya miaka mitatu ntaanza kupata mavuno yaani nitazalisha mara mbili yake sijutii uamuzi huu kwakuwa nimekuwa nikipata hasa kubwa kwakupata mavuno kidogo yasiyo na tija”
“Yaani nina michikichi mingi kwenye eneo la hekali nne lakini Napata mavuno kidogo sana lakini ninamategemeo makubwa na hii mbegu mpya aina ya tenera ambayo nimepata kutoka tari kihinga”
“Uvunaji haukuwa mzuri na tulikuwa tunavuna mara mbili kwa mwaka kwakuwa tulikuwa tukipata mavuno kidogo ndio maana tulipoona ujio wa mbegu mpya kwetu tuliona ni mkombozi na tunaamini kuwa tutafanikiwa kwakuwa tumeshaanza kuona matunda” alisema Juma
0 Comments