RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali na wa Kampuni ya Vigor, wakati akiwasili katika viwanja vya Kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja kuhudhuria Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad ( S.A.W) yaliyofanyika jana usiku,26-10-2021.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika Qiyaam wakati ukisomwa mlango wa nne wa Maulid ya Barzanj kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) akiwa mgeni rasmin katika Maulid hayo yalioandaliwa na kampuni ya Vigor A Turky’s Group Companies, yaliofanyika katika viwanja vya kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na (kushoto kwa Rais) Mhe Taufiq Turky na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali.
SAYYID Maalim Abubakar Bin Said akisoma akisoma dua ya barzazanji wakati wa Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad(S.A.W) yalioandaliwa na kampuni ya Vigor A Turky's Group Companies , yaliofanyika katika viwanja vya Kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi "B" Unguja
USTADH. Abdulrahaman Mwinyi Dedes Barzanj Mlango wan ne wakati wa Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, yalioandaliwa na kampuni ya Vigor A Turky’s Companies.
USTADH. Halfan Amran akisoma Mlango wa kwanza wakati wa hafla ya Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
USTADH Sayyid Abdulrahaman Al Habshy akisoma Quran Suratul Yasin wakati wa hafla ya Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yalioandaliwa na Kampuni ya ‘Vigor A Turky Group of Companies’ yaliofanyika jana usiku 26-10-2021 katika viwanja vya kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
0 Comments