Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la zima moto na uokoaji Mkoa wa Mwanza Abwene Mwakibete ameataja chanzo cha moto uliosabababisha bar ya the cask kuungua ni hujuma. mwandishi wa matukio daima Chausiku said anaripoti kutokea Mwanza
Mwakibete ameeleza hayo wakati akizungumuza na waandishi wa habari ofisini kwake na kueleza kuwa baada ya kutokea tukio hilo jeshi la zimamoto lilianza kufanya uchunguzi na kubaini chanzo hicho.
Ameeleza kuwa bado wanaendelea na Uchunguzi ili kufahamu waliohusika na Hujuma hiyo ya moto katika bar ya the cask na nini chanzo cha kuwasha moto huo.
"Tumeshashirikisha vyombo vingine vya usalama ili kuweza kutusaidia kufanya uchunguzi zaidi ili kufahamu chanzo cha tukio hilo" alisema Mwakibete.
Kwa upande mwingine ameeleza kuwa madhara yaliyotokea ni makubwa yaliyopelekea bar hiyo kuteketea na kuunguza vitu kwa asilimia kubwa.
Mwakibete ameeleza kuwa kutokana na bar hiyo kujengwa kwa mbao imepelekea kuungua kwa kiwango kikubwa.
"Mbao ni chakula kikubwa cha moto na ndio sababu iliyopelekea moto huo kusambaa kwa haraka sana" alisema Mwakibete.
Hata hivyo ameeleza kuwa kuteketea kwa bar hiyo kumesababishwa na kutotolewa taarifa kwa wakati na kupelekea kuungua kwa kiasi kikubwa.
" chanzo cha moto kinaweza kuwa chochote ila ukiwahi kutoa taarifa mapema kunusuru mali na maisha ya watu inawezekana na madhara yakawa madogo.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuhakika wanatoa taarifa mapema pindi wanapoona majanga ya moto yanatokea.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2019 bar hiyo iliwahi kuwaka moto na kuzimwa kwa haraka na kutosababisha madhara yeyote yale.
0 Comments