Header Ads Widget

MWANAJESHI AWATUPA MAHABUSU WAZAZI WAKE


Mwanajeshi Commandoo nchini Nigeria ameamua kuwasweka ndani Wazazi wake yaani Baba na Mama baada ya kugundua kuwa Pesa kibao alizokuwa akiwatumia akiwa masomoni nchini Italy kwa ajili ya ujenzi wa nyumba walizifuja.


Mwanajeshi huyo Capt Brian ambaye alikuwa masomoni nchini Italy kwa miaka sita ameeleza kuwa alikuwa akiwatumia pesa za kujikimu na pia kusomesha wadogo zake lakini jambo la kushangaza Wazazi wake hao walikuwa wakimtumia picha feki kuwa ndiyo nyumba yake hadi alipokuja kugundua utapeli huo majuzi aliporejea kutoka masomoni.


Capt Brian aliamua kuwasweka mahabusu Baba na Mama yake na kuamuru kuwa yeyote ambaye angewawekea dhamana basi angekabiliana naye na kwamba baadae atawafungulia mashtaka ambapo endapo watapatikana na hatia wanaweza kwenda jela miaka kumi kwa utapeli huo.


Je unadhani uamuzi wa Capt Brian ni SAWA? 

#JAYSADIAN__

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI