Header Ads Widget

MAABARA YA KUHIFADHIA MAZAO YA HORTICULTURE YASAIDIA KUONGEZA AJIRA KWA WAKULIMA

Zaidi ya wakulima 300 wameendelea kunufaika na teknolojia ya uhifadhi wa mazao ya horticulture na kusaidia kubaki kama yalivyotoka shambani na kusafirishwa katika masoko ya nje ikiwa hali hiyo imeongeza uzalishaji pamoja na ajira kwa wakulima.Mwandishi wa Matukio Daima Teddy Kilanga anaripoti toka Arusha 

Akizungumza mmoja wa wakulima wa zao pilipili mkoani Arusha,wakati wa uzinduzi wa kituo cha utoaji huduma wa mazao ya horticulture Edith Banzi alisema kupitia kituo hicho ameweza kunufaika na utunzaji wa mazao yake kupitia gari la kisasa lenye mahabara ya kutunza mazao ya horticulture na kubaki kama yalivyotoka shambani kwani hapo awali alishindwa kusafirisha mazao yake nje ya nchi kutokana na mazao hayo kuaribika kwa kukosa ubora unaotakiwa.

"Nilikuwa nikivuna mazao yangu yanaharibika haraka kwani soko la nje la  pilipili wanahitaji bidhaa hiyoikiwa bado na kikonyo chake kibichi lakini tangu kuanzishwa kwa kituo hiki kimetusaidia sana kwani maabara hiyo inahifadhi mazao yetu yanabaki kama yalivyotoka mashambani hivyo tumeongeza uzalishaji pamoja na ajiri kwa wanawake na vijana zaidi ya 250,"alisema Banzi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taha, Dkt.Jacqueline Mkindi alisema katika kuhakikisha wakulima wanaongeza uzalishaji wa mazao ya horticulture Taha kupitia kituo hicho imefanikiwa kutoa mafunzo ya mbinu bora za kilimo  na teknolojia kwa wakulima zaidi ya 300 huku asilimia 40 ni wanawake.

"Lakini tangu kituo hicho kianzishwe vitalu vya miche zaidi ya  laki 370 aina ya habanero imeweza kuzalishwa na kusambazwa katika mikoa ya Kilimanjaro pamoja ma Arusha nakufanikiwa kuzalisha tani 526 za mazao yenye thamani zaidi  sh.milioni 298 ambapo fedha hizo zimekwenda kwa wakulima,"alisema Dkt.Mkindi.

Dkt.Mkindi alisema  vilevile uzalishaji wa miche  laki nne na elfu sitini ya mazao ya pilipili kali na tikiti chungu ,kiasi cha tani 62 za tangawizi,maharage machanga,pilipili mbuzi na nyanya zimeweza kufungashwa kutoka katika kituo hicho na kusafirishwa katika masoko ya nje ya nchi ya Tanzania.

Aliongeza kuwa kiasi cha tani nne za maharage machanga kimevunwa katika mashamba ya mavuno na kusarishwa kwenda kwenye masoko ya kimataifa.

Mkurugenzi Mkaazi wa UNDP,Christine Musisi aliipongeza Taha kwa kuwakusanya wakulima wa mazao ya horticulture katika kuwaelimisha na kuwasaidia kuwatafutia masoko ya ndani na nje ya nchi ili kumuinua kiuchumi kwani sekta hiyo inaongeza ajira  kusaidia watu kupata mlo kamili.

Naye Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye ni Afisa kilimo mkoa wa Arusha,Daniel Loiruck alisema sasa hivi wapo kwenye mikakati ya kuhakikisha wakulima wa mkoa huo wanabadilika kutoka kwenye kilimo cha mazoea na kuongeza tija ,ajira na kuwa na uhakika wa masoko husika

Awali akizindua  kituo hicho kilichosheheni vifaa vya aina mbalimbali,Naibu waziri wa Kilimo ,Hussein Bashe aliagiza ofisi ya Mkuu wa mkoa Arusha na wilaya Arumeru kuharakisha mikakati ya ufufuaji wa mashamba saba  yaliyosimamisha uzalishaji  maua,mboga na matumda ili kuongeza ajira na mapato serikalii

Alisisitiza kuwa ni vyema ofisi ya mkoa wa Arusha na wilaya wakaweka mikakati ya haraka na kukaa pamoja na wizara yenye dhamana na kuandaa nyaraka ambayo itahihamasisha wizara ya fedha kwa ajili ya kuweza kutafuta wawekezaji wa mashamba hayo saba ya maua ,mboga na matunda ili kuendelea na uzalishaji wake.

"Kwa kufufua mashamba haya yatasaidia kuongeza ajira na kuwasaidia vijana na wanawake katika kujikwamua kiuchumi na kutoka katika hali ya umasikini kwani mazao haya ni ya kisasa na yanajiuza kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandaoni na serikali imeweka nguvu katika kuhakikisha wakulima wa mazao ya horticulture wanapata masoko hasa ya Kimataifa,"alisema.

Aidha Bashe alisema pamoja na wakulima wa mazao hayo kupata elimu bado wanakabiliwa na changamoto ya kutokufahamu miundombinu ya masoko ikiwemo gari la baridi linalosaidia kubakisha mazao katika ubora wake wa shambani.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI