Header Ads Widget

MLIPUKO WA MABOMU WAUA WANAJESHI NCHINI SYRIA

Watu wasiopungua 13, wengi wao wakiwa wanajeshi, wameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulio la basi katikati mwa mji wa damascus.

Mabomu mawili yalilipuka wakati basi lililokuwa limebeba wanajeshi lililopita chini ya daraja mjini Damascus ambapo milipuko hiyo ilisikika sehemu kubwa ya mji mkuu wa Syria na kutikisa baadhi ya maeneo ya mji huo.

Kifaa cha tatu cha kulipuka kiligunduliwa na kuteguliwa na wataalamu wa kijeshi, kulingana na Shirika la Habari la Serikali Syria (SANA)japokuwa mamlaka nchini Syria haijaeleza ikiwa shambulio hilo lilikuwa la kujitoa muhanga au bomu lililofyatuliwa kwa mbali.

Picha zilizorushwa na vyombo vya habari zinaonyesha basi lililoteketezwa kwa moto na milipuko hiyo baada ya maofisa wa zimamoto kuingilia kati.

Tangu wanajeshi wa  serikali ya Syria walipopata tena udhibiti wa mji wa Damescus na viunga vyake takribani miaka mitatu iliyopita hali ya utulivu imetawala na mashambulio kama hayo ni nadra kutokea ambapo shambulio la mwisho lililotokea mwaka mmoja uliopita wakati mufti wa kusini mwa mkoa wa Damascus Adnane al Afy-ouni, alipouawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa katika gari lake huku ikielezwa kuwa shambulio hilo lilitokea Qoudsaya, kitongoji cha karibu cha Damascus.

Shambulio hilo la jana linatajwa kuwa ni tukio la kipekee na ni uvunjaji wa mfumo wa usalama uliowekwa katika mji mkuu wa Syria na viunga vyake..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI