Header Ads Widget

MGANGA WA KIENYEJI AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUMBAKA MTEJA.

Mahakama ya Mkoa Chake Chake imemuhukumu Mshitakiwa Issa Abdalla Haji(41) mkazi wa Shehia ya Wawi Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 30 pamoja na kulipa fidia ya shilingi milioni moja za Kitanzania baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kubaka. mwandishi wa matukio daima Hassan Msellem anaripoti kutoka Pemba. 

Hukumu hiyo imetolewa jana Octoba 20 na hakimu wa mahakama ya Mkoa Chake Chake Luciano Makoye Nyengo baada ya mtuhumiwa kukiri kutenda kosa hilo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo.

Mwendesha mashtaka Ali Amour Makame kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ameeleza kwamba mshtakiwa alidaiwa kumbaka mwanamama mmoja mwenye umri wa miaka 39 jina limehifadhiwa Octoba 11 mwaka huu wakati mshitakiwa alipomtaka mama huyo wafanye mapenzi ikiwa ni miongoni mwa masharti ya dawa itakayoweza kumtoa mume wake rumande ambako anashikiliwa kwa tuhuma ya kesi ya jinai ndipo mganga huyo alipomuingilia mama huyo bila ridhaa yake jambo ambalo ni kosa kisheria. 

Mshitakiwa alipotakiwa kujibu shitaka hilo bila ya kupepepsa macho alikiri kutenda kosa hilo, ndipo hakimu wa mahakama hiyo hakimu Nyengo alipomuamuru mshitakiwa huyo kutumikia miaka 30 chuo cha mafunzo na kumlipa mlalamikaji fidia ya shilingi milioni moja ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hizo.

‘’kwa mujibu wa sheria No. 6 ya mwaka 2018 kifungu cha 108 kifungu kidogo cha 1, kifungu kidogo cha 3, mabano (b) sheria ya makosa na adhabu Zanzibar nakuhumu kwenda chuo cha mafunzo miaka 30 pamoja na kulipa fidia ya shiling milioni moja ili iwe fundisho kwako na kwa wengine wenye tabia kama hizi’’ alieleza hakimu huyo

Ikumbukwe kuwa mwanaume huyo yuko nje kwa dhamana ambapo anakabiliwa shitaka la tuhuma ya wizi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI