Mkurugenzi wa kampuni ya Rick na mzaliwa wa kata ya Bomalang'ombe kijiji cha Ng'ingula wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Brian Kikoti ameahidi kutatua changamoto ya maji katika shule ya sekondari Ipeta .
Kikoti akiwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne shule ya Sekondari Ipeta iliyoko kata ya Bomalang'ombe alitoa ahadi hiyo baada ya wahitimu wa kidato cha nne shuleni hapo kwenye risala yao kueleza changamoto hiyo ya maji
"Kama gharama za kuchimba kisima ni hizi basi mimi Nasema kuanzia kesho mafundi wafike hapa na kisima kianze kuchimbwa"
Kuhusu taaluma shuleni hapo kikoti aliwataka walimu, wazazi na wanafunzi kushirikiana na kila mmoja kutimiza wajibu wake ili kuimarisha ufauru wa wanafunzi shuleni hapo.
Akielezwa kuhusu suala la motisha kwa wahitimu wa kidato cha nne, Kikoti ameahidi kutoa kiasi cha shilingi laki tatu kwa kila mwanafunzi atakayepata Daraja la kwanza katika matokeo ya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka huu na kwamba hata kama watakuwa zaidi ya arobaini atawapa wote.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo pamoja na Diwani viti maalum, wazazi pamoja na wanafunzi wamempongeza Kikoti kwa kwa moyo wake wa kujitolea na kukumbuka kuchangia maendeleo ya nyumbani aliko zaliwa.
Kikoti ametoa ahadi hiyo huku zikiwa zimepita siku chache tu baada ya kuchangia ujenzi wa jengo la ofisi ya kata ya Lugalo wilayani Kilolo, ambapo aliahidi kuendelea kuchangia maendeleo maeneo mengi katika wilaya ya Kilolo na mkoa wa Iringa kwa ujumla.
Kwa upande wao wageni walioambatana na Kikoti ,Baraka Kimata diwani mstaafu kata ya Kitwiru na Bw Osca Ndale wamemuunga mkono kwa kuchangia mifuko 10 ya saruji ambapo waliahidi kumkabidhi mkuu wa shule wakati wowote atakapo kuwa tayari kuichukua.
0 Comments