MTANDAO wa Madeni na Maendeleo Tanzania (TCDD), umeliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka utaratibu mzuri wakati wa kukopa fedha kwa kuainisha matumizi sahihi ya mkopo unaotaka kuchukuliwa na Serikali. mwandishi wa matukio daima Fatma Ally anaripoti kutokea Dar Es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam J Mkurungezi wa TCDD, Hebron Mwakagenda katika mkutano uliokutanisha viongozi mbalimbali wa dini pamoja na wadau wa Maendeleo, sambamba na uzinduzi wa ripoti ya hali ya deni iliyolenga kujadili taarifa kuhusu deni la taifa na Maendeleo .
Amesema kuwa, kinachofanyika kwa sasa, Waziri wa fedha kwenda Bungeni kusoma hotuba yake akieleza kuwa atakusanya kiasi fulani ndani na kukopa kiasi fulani, mfumo huo bado unamapungufu kinachotakiwa ni kutoa maelezo kuwa fedha hizo zinakwenda sehemu fulani na zimetoka sehemu fulani.
Aidha, amesema kupitia mfumo huo sasa, bunge linapaswa kuizinisha kwa kutoa ruhusa ya kukubali ama kukataa, huku Waziri wa fedha akipeleka mapendekezo kwa kamati kwa kueleza kuwa anataka kukopa sehemu fulani kwa ajili ya kitu fulani.
"Bunge ndilo linapaswa kukopa kwa niaba ya nchi mikopo mbalimbali ya ndani na nje Ili kusimamia uwajibikaji wa mikopo hiyo badala ya utaratibu wa sasa wa Waziri wa fedha kukopa kwa niaba ya nchi"amesema Mwakagenda
Ameongeza "Baada ya Waziri wa fedha kueleza kuwa fedha hizo zitakopwa wapi kwa ajili ya kitu gani ndipo bunge nzima linakaa na kujadili kwa kutoa hoja za kukubali au kukataa,".
Akizungumzia kuhusu hali ya deni ya kwa nchi za Afrika Mashariki amesema hali ni mbaya zaidi katika nchi ya Kenya, Uganda, na Rwanda huku Tanzania ikionekana kuwa na unafuu.
Ameeleza kuwa, nchi hizo zimekuwa zikiendelea kukopa na kupata maendeleo kutokana na fedha zinazochukuliwa zaidi zikijielekeza kwenye kujenga Miundombinu, Madarasa,Madaraja,Reli, pamoja na Barabara ambapo fedha nyingi hutumika kama zilivokusudiwa.
"Uchumi wa Tanzania umebadilika kwa sasa, awali kulikuwa na mfumo wa kijamaa ambapo serikali ilikuwa ikiendeshwa kwa kitu, kwa Kenya mfumo wao umekuwa ukiendeshwa na sekta binafsi jambo ambalo limepelekea Uchumi wao kukua kwa haraka,"amesema Mwakagenda.
Mwakagenda amesema Nchi ya Tanzania imekuwa na rasilimali nyingi huku kwa Sasa ikija kwa kasi zaidi na kusisitiza kuwa kinachotakiwa kwa sasa serikali ni kuwa na nidhamu ya ukopaji.
Awali Mwenyekiti wa TCDD, Piter Maduki akizungumza mara baada ya kuzindua taarifa hiyo amesema kwa sasa deni la Taifa ni imilivu ambapo aliwaomba watanzania kutambua kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya manufaa ya wote hivyo ni vyema kutumika vizuri katika utekelezaji na hatimaye kuleta mafanikio makubwa zaidi.
Akiwasilisha taarifa ya ripoti hiyo Mwalimu wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu huria Dkt Felician Mutasa amesema kukopa sio dhambi kwani hata nchi tajiri zimekuwa zikikopa huku akieleza ni jambo la kawaida katika mifumo ya kiuchumi.
Amesema kinachotakiwa kuzingatia fedha zinapokopwa ni vema zikaelekezwa katika miradi iliyokusudiwa zaidi.
Hata hivyo, ripoti hiyo pia imependekeza kuwepo kwa wigo mpana wa Kodi kwani ndo kitu pekee kitakachoifanya Serikali kujiendesha kuliko msaada na mikopo hivyo ni vema serikali ikaweka nguvu zaidi.
0 Comments