Header Ads Widget

PROF ANANGISYE AWATAKA WAHITIMU UDSM WASISUBIRI KUAJIRIWA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) Prof William Anangisye  amesema licha ya kupitia changamoto ya ugonjwa wa UVIKO 19, lakini chuo hicho kimeweza kuongeza fedha za utafiti kutoka shill mill 712,800,000 kwa mwaka 2018 hadi kufikia shill bill 3,150,000,000 kwa mwaka 2021. mwandishi wa matukio daima Fatma Ally anaripoti kutokea Dar Es Salaam

Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika mahafali ya 51 awamu ya tatu, ambapo alisema lengo ni kuboresha na kuongeza ufanisi, ambapo mwaka huu chuo hicho, kimeamua kuwa, kati ya fedha hizo, shill mill 700 zitatumika kwa ajili ya uvumbuzi ambapo fedha hizo zinatokana na vyanzo vya ndani .

Aidha, amewataka wahitimu hao kutumia elimu yao kama ushawishi kwa watu wote, ili wawe chachu ya mabadiliko katika jamii, huku akiwataka ambao wanarudi kwenye vituo vyao vya kazi watakua chachu ya kuongeza tija katika majukumu yao ya kila siku pia kuwa uzalendo.

Hata hivyo, amewataka wahitimu hao wasisubiri kuajiriwa na Serikali bali wawe wepesi kuangalia ni wapi ujuzi wao unaweza kutumika kwa ufanisi zaidi hata kama itabidi wafanye kazi za kujitolea, kwa kufanya hivyo watajenga kujiamini, ujuzi na mchango wao utatambuliwa na kuinufaisha jamii.

Alisema kuwa, mahafali ya 51 katika awamu ya pili na ya tatu wanafunzi 4,298 wamehitimu na kutunukiwa Shahada, Stashahada na Astashahada mbalimbali ikiwemo ndaki ya Uhandisi naTeknolojia, ndaki ya Insia, ndaki ya Teknolojia ya habari na mawasiliano, shule kuu ya Biashara, Madini na Jiosayansi na Taasisi za kiswahili.

Ameongeza kuwa, pia wapo wahitimu kutoka ndaki ya Sayansi za kilimo, Teknolojia ya chakula, Sayansi Asilia na Tumizi, Sayansi za jamii, Shule kuu ya uchumi, Sayansi Akua, na Teknolojia ya uvuvi, Shule kuu ya Sheria, Shule ya Uandishi wa habari na mawasiliano ya Umma (SJMC) pamoja Taasisi ya Taaluma za Maendeleo IDS.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Jaji mstaafu  Damian Lubuva amesema baraza linaendelea kutoa ushauri na maelekezo mbalimbali wa Chuo Ili kuhakikisha kuwa lengo la utoaji wa elimu, utafiti a ushauri wa kitaalamu linafanikiwa ikiwemo kuendelea kusimamia uharakishwaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya chuo Ili kuboresha utoaji huduma ikiwemo elimu bora.

Aidha amewataka wahitimu hao kuwa werevu katika kuzikabili changamoto za maisha watakazokumbana nazo, huku akiwataka wawe na Umoja na mshikamano katika kila Jambo watakalolifanya Ili kutafuta fursa za kujiendeleza kimaisha .

Jumla ya wahitimu 4,298 wametunukiwa, Shahada, Stashahada na Astashahada na Mkuu wa Chuo hicho, ambae pia ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete katika mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jiijini Dar es salaam.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI