Header Ads Widget

MBUNGE PROF. NDAKIDEMI AOMBA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI KUPEWA KIPAOMBELE BAJETI YA BARABARA.

 



NA WILLIUM. PAUL,  Moshi. 


MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi amesema kuwa, changamoto ya mkoa wa Kilimanjaro ni barabara na kuomba jimbo lake kupewa kipaombele pindi mgawanyo wa fedha unapofanyika kutokana na barabara nyingi kutopitika hasa kipindi cha mvua.

 

Prof. Ndakidemi ametoa kauli hiyo leo wakati wa ziara ya kikazi ya Rais Samia Suluhu Hasani mkoani Kilimanjaro akizungumza na wananchi katika viwanja vya chuo kikuu cha Ushirika mjini Moshi.


Prof. Ndakidemi alisema kuwa, ipo barabara ya Mabogini - Tpc – Kahe ambayo ipo katika Ilani ya Uchaguzi ambapo imekuwa haipitiki na kusababisha kero kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayona kumuomba Rais Samia kukarabatiwa kwa barabara hiyo.

 

“Ipo barabara ya Kiboroloni – Suduni – Kidia nayo ipo kwenye ilani ya uchaguzi ya ccm tunaomba nayo iweze kujengwa kwa kiwango cha lami hizi zote ni barabara zilizopo kwenye Ilani yetu” alisema Prof. Ndakidemi.

 

Mbunge huyo alisema kuwa, ipo pia changamoto ya miundombinu ya umwagiliaji kuchoka na kumuomba Rias Samia kuboreshwa kwa miundombinu hiyo ili kuifanya Kilimanjaro kurudi kwenye kulisha Tiafa chakula.

 

Aliongeza kuw, Wananchi wa vijiji vinavyozunguka mlima Kilimanjaro wamekuwa na mgogoro na hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA) kuhusu eneo la Nusu maili na kumuomba Rais Samia kuwaruhusu wananchi kuendelea kulinda eneo la Nusu maili.

 

Mwisho…

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI