Header Ads Widget

MADIWANI WANAWAKE KILIMANJARO WAFUNDWA KUELEKEA KUSIMAMIA FEDHA ZA MAMA SAMIA.

 


NA WILLIUM PAUL, Moshi.

MADIWANI nchini wametakiwa kusimamia fedha zitakazoletwa na Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo bila kumuangalia mtu usoni ili thamani ya fedha iendane na thamani ya mradi.


Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi wakati wa uzinduzi wa semina ya Madiwani Wanawake wa mkoa huo iliyofanyika katika ukumbi wa Uhuru hostel mjini Moshi.



Amesema kuwa, Rais Samia Suluhu Hasani amedhamiria kukuza maendeleo kwa kuleta fedha nyingi hivyo Madiwani wanajuku kubwa la kusimamia fedha hizo ili kutumika kama zilivyokusudiwa huku wakitambua kuwa miradi hiyo ni kwa ajili ya wananchi wanaowaongoza.


“Leo mnapata semina ni vizuri mkayatumia mafunzo haya kwenda kuhoji fedha za maendeleo zinazotolewa na serikali na lengo la chama na serikali ni kuhakikisha tunawatumikia wananchi na kumaliza kero na matatizo yanayowakabili” alisema Boisafi.


Mwenyekiti huyo amesema kuwa, kila Diwani anajukumu la kumuunga mkono Rais Samia na kudai kuwa endapo wakianza kufikiria tofauti watapoteza mwelekeo na kumuunga huko mkono kutapelekea uchaguzi ujao mwaka 2025 kuwa mwepesi na rahisi kwa chama cha mapinduzi.



Akizungumzia swala la Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwakani, Boisafi amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa ili kuisaidia Serikali kutambua idadi ya wananchi wake ili iweze kuwahudumia kwa vitendo.


Amesema kuwa, kazi ya kiongozi ni kuonyesha njia na kuwataka madiwani kuwahamasisha wananchi kushiriki katika Sensa huku wakiwaeleza faida za wao kuhesabiwa.


Mwenyekiti huyo pia amezungumzia swala la mikopo ya kinamama, vijana na watu wenye ulemavu inayotolewa na halmashauri asimilia kumi ya mapato ya ndani aliwataka Wakurugenzi wa halmashauri kutambua kuwa fedha hizo sio hiari bali ni lazima huku akitoa wito kwa madiwani kuhakikisha vikundi vinavyokopeshwa vinarejesha ili fedha hizo ziwanufaishe wengine.


Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Ummy Nderiananga amesema kuwa, lengo la Semina hiyo ni kuwajengea uwezo madiwani kuhusu haki, sheria na wajibu wa viongozi katika maeneo yao.



Naibu Waziri Ummy amesema kuwa, amesukumwa kuwajengewa uwezo madiwani hao kutambua sheria na kanuni zitakazoweza kuwasaidia katika kutimiza wajibu wao hasa katika utoaji wa mikopo ya halmashauri hivyo mafunzo haya yatawapa mwaka katika kufwatilia na kusimamia fedha hizo.


“Rais Samia anapeleka fedha nyingi katika kata zetu hivyo mafunzo haya yatawasaidia madiwani wa mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha wanafwatilia na kusimamia fedha hizo ziweze kutekeleza lengo lililokusudiwa” amesema Naibu Waziri Ummy.


Ametumia pia nafasi hito kutoa wito kwa Wakurugenzi wa halmashauri nchini kuendelea kutoa mikopo kwa watu wenye ulemavu ambayo ni asilimia mbili ya mapato ya ndani ambapo amesema kuwa mpaka sasa taarifa kutoka Tamisemi jumla ya Bilioni 12.9 zimeshatolewa kwa watu wenye ulemavu.


Ameitaka Jamii kuendelea kuwathamini watu wenye ulemavu kama ambavo Rais Samia anavowapenda na ametoa fedha kwa ajili ya kujenga mabweni 50 ya watu wenye ulemavu hali ambayo itachochea ufaulu na kuzitaka kamati husika kuhakikisha wanasimamia vizuri fedha hizo.


Semina hiyo yenye kauli mbiu ya “sisi madiwani wanawake Kilimanjaro tunaungana na wewe Rais Samia Suluhu Hasani kuendelea kuchapa kazi” imetajwa kuwa chachu ya kuongeza mafanikio na kukuza uchumi wa mkoa wa Kilimanjaro.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI