Header Ads Widget

BUSTANI YA MANISPAA YA IRINGA IBORESHWE

Baadhi ya maeneo ya bustani ya Manispaa ya Iringa yalivyo Kwa sasa

 Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Iringa wameeleza kusikitishwa na hali ya bustani ya Manispaa ya Iringa na kuomba uongozi wa Manispaa kuchukua hatua ya kunusuru bustani hiyo .

Wakizungumza na matukio Daima media Leo Yohana Ndelwa na John Sanga walisema eneo hilo ndilo eneo pekee Kwa wananchi kufika kupumzika ila mazingira yalivyo Sasa hayavutii mtu kupumzika.

Hivyo wameshauri kama Kuna mwekezaji eneo hilo ajitahidi kupendezesha mazingira ya bustani hiyo kama ilivyokuwa zamani.

Mwanzoni mwekezaji alionesha mwelekeo mzuri wa kutengeneza eneo hilo ila Kwa Sasa mazingira si rafiki hivyo maboresho yanahitajika zaidi .


Matukio Daima Media tutaendelea kuleta mwendelezo wa taarifa hii hii Kwa kumtafuta mwekezaji na uongozi wa Manispaa ya Iringa ya Iringa ili kujua Mpango wao Katika eneo hilo 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI