Header Ads Widget

KWANINI BADO WANAWAKE WANAFUNGWA UZAZI KWA NGUVU BILA HATA KUJUA?

Getty images

"Nisingekubali kufungwa kizazi. Kile kilichofanyika kwangu ni ukatili mkubwa. Sasa najihisi sina maana wala thamani. Nimekufa," anasema Zisilo Dludlu.

Nyaraka za hospitali zinaonyesha kuwa yeye mwenyewe alisaini makubaliano ya kufungwa kwa kizazi chake. Kulingana na madaktari, mwanamke huyo alikuwa tayari amejifungua kwa njia ya upasuaji (CS), n ani utaratibu wa kawaida nchini Afrika Kusini kuwafunga kizazi wanawake baada ya kupata watot watatu kwa njia ya upasuaji ili kuimarisha afya zao.

Wanawake wanaotoka katika mazingira magumu, wenye virusi vya HIV, ambao hawajasoma au wanaoishi chini ya viwango vya umasikini, mara nyingi husaini idhini ya kufungwa kwa vizazi bila kufahamu ni nini hasa wanachokifanya.

Zishilo anakana kwamba alitoa idhini na anaamini kwamba alifungwa kizazi kwa nguvu, ikiwa ni pamoja na kwasababu anaishi na virusi vya HIV.

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Zishilo anakana kwamba alitoa idhini na anaamini kwamba alifungwa kizazi kwa nguvu, ikiwa ni pamoja na kwasababu anaishi na virusi vya HIV.

"Kitu cha aina hii hutokea kwa wanawake wengi sana. Hasa wanawake weusi, masikini wanaoishi vijijini, ambo wengi wao wanaishi na virusi vya HIV. Wanasaini, "anasema mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya afya, Dkt Tlaleng Mofokeng.

Zishilo Dludloo na wanawake wengine wamewasilisha malalamiko yao katika Kamati ya Afrika Kusini ya usawa wa jinsia. Lakini uchunguzi uliofanyika mwaka jana haujafika kokote hadi sasa. Kamati hiyo haijakiri wazi kwamba haki za wanawake ziliiuka vibaya.

Wizara ya afya ya Afrika Kusini haikujibu Ombi la BBC la kuzungumzia kuhusu suala hili.

Getty images

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Wanawake wengi hufungwa vizazi bila kujua mara wanapomaliza kujifungua

Hatahivyo, kitendo cha kuwalazimisha wanawake kufungwa uzazi hakifanyiki kwa wanawake wenye virusi vya HIV pekee kote duniani.

Kwa mfano ripoti ya taasisi ya Global Public Health inaelezea kisa cha wanawake wanne wa jamii asilia ya chini Canada ambao walisema kuwa walilazimishwa kufungwa vizazi vyao baina ya mwaka 2005 na 2010.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa pia inaelezea Ushahidi kwamba wanawake wa Romani katika Jamuhuri ya Czech , Hungary na Slovakia walilazimishwa kukubali kufungwa vizazi vyao wakati walipojifugua watoto.

Mmoja wao alilazimika kutibiwa baada ya kuvuja damu nyingi wakati wa ujauzito.

Aliambiwa kwamba mtoto wake amefariki na kwamba alihitaji kufanyiwa upasuaji wa haraka ili kumuondoa mtoto. Wakati alipokuwa kwenye meza ya upasuaji, aliambiwa asaini fomu ambayo ilikuwa vigumu kwake kuisoma, iliyoandikwa kwa kilatini.

Baada ya kufanyiwa upasuaji, mwanamke huyo alimuuliza daktarin ni lini anaweza kupata tena ujauzito tena. Daktari alikiri kwamba wakati alipofanyiwa upasuaji alifungwa kizazi, n ani hapo ndipo alipogundua kwamba alikuwa amesaini idhini ya kufungwa kizazi katika chumba cha upasuaji bila kujua.

Tlaleng Mofokeng anasema mifano ya kufugwa kizazi bila kutaka imegundulika katika maeneo yote duniani, sio tu Afrika Kusini. Zaidi ya hayo kuna sheria katika nchi mbali mbali zinazohalalisha kuwafunga vizazi wanawake kwa nguvu, na kuwaacha hawana la kufanya.

Nchini Japan, kwa mfano, kufungwa kwa vizazi ni mojawapo ya masharti kwa ajili ya upasuaji wa kurekebisha jinsia kwa watu waliozaliwa na jinsia mbili. Iwapo watakataa kufungwa uzazi, huzuiwa kufanyiwa upasuaji huo.

Na nchini India, serikali hutoa msaada wa pesa kwa familia ambazo hazina watoto zaidi ya wawili.

Kwa mfano, ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kwamba watu ambao walikataa kutoa vyeti vya kufungwa uzazi walinyimwa chakula kwa ajili ya watoto wao.

Wataalamu wanauita ubaguzi katika utoaji huu wa marupurupu, unawalazimisha watu wenye kipato cha chini kukubali kufanyiwa upasuaji wa kufunga vizazi vyao na kutoweza kupata fursa nyingine ya kupata watoto wanapohitaji kufanya hivyo.

Sheria ya Uhispania na zile za kigeni huruhusu kufunga vizazi vya watoto wenye matatizo makubwa ya kiakili.

Majimbo kumi na matano ya Marekani yanasheria ya kufanya upasuaji wa kufunga kizazi wanawake wenye matatizo fulani ya afya. Umasikini unaweza kuwa ''hali ya awali'' ya kumfanya mtu afunge uzazi. Ripoti inaelezea kuhusu mwanamke Mmarekani ambaye aliwasilisha mashitaka mahakamani dhidi ya hospitali mwaka 2009 baada ya kufungwa uzazi bila idhini yake wakati alipojifungua kwa njia ya upasuaji (CS)

laleng Mofokeng anasema: " Kazi yangu ni kuyakumbusha mataifa kwamba yana jukumu la kufanya uchunguzi wa haki kuhusu visa vya kuwafunga uzazi wanawake kwa lazima na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika ."

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

laleng Mofokeng anasema: " Kazi yangu ni kuyakumbusha mataifa kwamba yana jukumu la kufanya uchunguzi wa haki kuhusu visa vya kuwafunga uzazi wanawake kwa lazima na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika ."

Umoja wa Mataifa unasema kuwa kuwafunga kizazi wanawake kwa lazima au kuhusika katika mpango kunapaswa kuchukuliwa kama aina ya ukatili.

Wataalamu wa Umoja huo wanatoa wito kwa serikali za mataifa mbali mbali kurekebisha sheria na kuacha kutumia ufungaji wa uzazi kama kigezo cha kupokea vifaa au usaidizi tiba.

"Ukatili huu na upasuaji wa kinyama, unawadhalilisha wanawake.Hatupaswi kuruhusu kitendo hiki kiendelee kuhalalishwa kisheria na kutowaadhibi wahusika," anasema Mjumbe maalum wa Umaija wa mataifa wa masuala ya haki za afya Dkt. Tlaleng Mofokeng.Chanzo BBC


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI