Mbegu za viazi lishe zaidi ya laki nane na themanini zimesambazwa kwa wakulima katika mikoa mbalimbali nchini ili kuhamasisha watanzania kuanza kutumia viazi hivyo kwa ajili ya kuboresha afya nchini. mwandishi wa matukio daima anaripoti kutoka Tabora
Akizungumza ofisini kwake Kaimu Mkurugenzi wa Tari kituo cha Tumbi Dr Emmanuel Mrema amesema kuwa Mwaka jana walisambaza mbegu laki 880, ambapo mbegu hizo zimesambazwa kwa mkoa wa Katavi pekee ili kuhamasisha ulimaji wa viazi lishe nchini.
“Sio hivyo tu kwa Tabora tumesambaza kwenye zahanati mashuleni bure ili watu waweze kupata mbegu hizi lakini pia tunatoa elimu ili watu waone umuhimu wa kutumia viazi lishe na mazao mengine” alisema
“Tunahitaji viazi lishe kwa afya ya macho na kuboresha afya zetu wenyewe sio watoto tu hata watu wazima ni viazi ambavyo vinafaa kwa afya” Dr Mrema
Kwa upande wake Mtafiti wa Kituo cha Utafiti Tari Tumbi Tabora Matha Ndelemba alisema kuwa kuwa viazi lishe vinafaa kwa afya za watoto chini ya miaka mitano, wanawake wanaonyonyesha na wajawazito.
“Tunahamasisha wananchi kuanza kulima viazi hivi ili kuweza kuboresha afya zao na Watoto na kupunguza utapiamlo hasa kwa watoto ambao wako shuleni vinafaa zaidi vina vitamin A yakutosha” alisema
“Tumesasmbaza mikoa mingi viazi lishe ili kuhakiksiha kuwa wakulima wanapta mbegu ili kuweza kuwafikia wakulima wengine” alisema Ndelemba
0 Comments