Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Ndungi katika Wilaya ya Moshi kwa tuhuma za kumuua ndugu yake, William Shoo kwa madai ya kukataa kuchangia nyama ya Sh1, 500 waliyonunua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema mauaji hayo yalitokea Oktoba 10, 2021 asubuhi baada ya marehemu kugoma kuchangia nyama hiyo waliyonunua.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, kabla ya mauaji hayo mtuhumiwa alinunua nyama kwa kushirikiana na marehemu ambapo walikula pamoja na walipomaliza kula marehemu alikataa kuchangia chochote ndipo ugomvi ukaanza.
Kamanda Maigwa amesema katika ugomvi huo, mtuhumiwa alimkata ndugu yake na kitu chenye ncha kali kichwani na kusababisha kifo chake.
0 Comments