Header Ads Widget

MBUNGE MTATIFIKOLO AWAPONGEZA WANACHAMA 240 JUU LA KIJIJI CHA ISIMANI AWACHANGIA TSH MILIONI 1

 


Mbunge wa jimbo la Ismani  Emmanuela Mtatifikolo amewapongeza wanachama wa kikundi cha Jukwaa la Kijiji cha Ismani Tarafani Kata ya Kihorogota kwa kuweza kushikamana hadi kufikia idadi ya wanachama 240 ambao wanashirikiana katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ya kijamii, kuimarisha umoja, mshikamano, ushirikiano na kuchangia kwa ajili ya maendeleo ya pamoja, kwani wamekua wa mfano katika vijiji vyote vya halmashauri ya wilaya ya Iringa.


Aidha, Mheshimiwa Mtatifikolo amewachagia wanachama hao kiasi cha shilingi milioni moja ili waweze kuendeleza jukwaa hilo kwa kununua vifaa mbalimbali ambayo vitawasaidia kuingiza kipato na kuongeza kipato cha mfuko wa jukwaa hilo, huku akiwaomba kuendelea kushirikiana na kupendana ili waweze kufika mbali zaidi.



Kwa upande wao wanachama wa jukwaa la Ismani Tarafani wamemshukuru Mheshimiwa Mtatifikolo (Mbunge) kwa kuwachangia kiasi hicho cha shilingi milioni moja ambacho kitawasaidia katika kuendeleza shughuli zao mbalimbali za jukwaa hilo huku wakimuahidi kuwa nae bega kwa bega katika kuleta maendeleo ya jimbo la Ismani.


Katika hafla ya sherehe hiyo Mheshimiwa Mtatifikolo amewakilishwa na Katibu wa ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ismani Ndugu Israel Chotamasege huku ikiuzuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na Chama.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI