Header Ads Widget

MAGAZETINI LEO JUMAMOSI NOVEMBA 7/2026:HUKUMU YA LISSU YAACHA MASWALI


div class="separator" style="clear: both;">

 

HIZI HAPA SHULE 10 ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI MTIHANI WA DARASA LA SABA 2026 MKOA IRINGA

 






NA MATUKIO DAIMA MEDIA, IRINGA

WAZAZI wa wanafunzi waliofanya mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi, darasa la saba mwaka 2026, katika Shule ya Good Victory iliyopo mjini  mkoani Iringa, wamepongeza matokeo mazuri yaliyopatikana na wanafunzi wa shule hiyo, ambapo wanafunzi wote 64 waliofanya mtihani huo wamefanikiwa kupata daraja A.

Wazazi hao wamesema matokeo hayo ni ishara ya ubora wa elimu inayotolewa shuleni hapo, juhudi za walimu katika kufundisha, usimamizi mzuri wa uongozi wa shule pamoja na ushirikiano uliopo kati ya walimu na wazazi katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.

Wakizungumza na Matukio Daima Media  kuhusu mafanikio hayo, Amina Sanga na John Ndelwa walisema wamefurahishwa na kuvutiwa na matokeo yaliyopatikana, wakieleza kuwa ni jambo la kujivunia kuona wanafunzi wote 64 wakifaulu kwa kupata daraja A.

Wamesema mafanikio hayo yanaonesha kuwa uwekezaji katika elimu, unapokwenda sambamba na nidhamu, maandalizi ya kutosha na ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya wanafunzi, unaweza kuleta matokeo makubwa na yenye manufaa kwa jamii.

Aidha, wazazi hao wameeleza kuwa matokeo hayo yanaongeza imani kwa wazazi na walezi wanaotafuta shule zenye uwezo wa kuwajengea watoto wao msingi imara wa kitaaluma, huku wakisisitiza umuhimu wa kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na taasisi za elimu katika kulea na kuandaa kizazi chenye maarifa.

Shule ya Good Victory iliyopo katika Manispaa ya Iringa imeonesha kiwango kizuri cha ufaulu kupitia matokeo hayo, ambapo wanafunzi wote waliofanya mtihani wamepata daraja la juu zaidi, jambo linaloweka alama muhimu katika historia ya maendeleo ya taaluma ya shule hiyo.

Kwa upande mwingine, mafanikio hayo yanaibua umuhimu wa kuendelea kuimarisha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, kuhakikisha walimu wanapata ushirikiano unaostahili na wanafunzi wanapata malezi yanayowawezesha kutumia vizuri vipaji na uwezo wao katika masomo.

Wadau wa elimu wamekuwa wakisisitiza kuwa mafanikio ya mwanafunzi hayajengwi na juhudi za upande mmoja pekee, bali yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya shule, wazazi na jamii kwa ujumla.

 Ushirikiano huo husaidia kufuatilia maendeleo ya watoto, kutambua changamoto mapema na kutafuta suluhisho zinazoweza kuboresha kiwango cha ufaulu.
Matokeo ya Good Victory ya mwaka 2026 yanatoa taswira ya matumaini kwa wazazi na wanafunzi wengine, huku yakiongeza matarajio ya kuona shule hiyo ikiendelea kudumisha kiwango hicho cha ufaulu katika miaka ijayo.

Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo, ni muhimu kwa shule kuendelea kuweka mikakati ya kudumisha ubora wa elimu, kuwajengea wanafunzi uwezo wa kufikiri kwa kina, ubunifu, maadili mema na kujiandaa kukabiliana na changamoto za hatua zinazofuata za masomo.

Kwa wazazi, mafanikio hayo ni faraja na uthibitisho wa umuhimu wa kuchagua mazingira bora ya elimu kwa watoto wao. Kwa wanafunzi waliofaulu, ni mwanzo wa safari nyingine ya kitaaluma inayohitaji bidii, nidhamu na kujituma zaidi.

Walisema ufaulu wa wanafunzi wote 64 kupata daraja A katika mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka 2026 ni mafanikio makubwa kwa Shule ya Good Victory, wazazi na jamii ya Iringa, huku ukiweka matarajio mapya katika safari ya kuimarisha ubora wa elimu mkoani humo.

Katika matokeo hayo shule zolizoingia kumi bora kwa mkoa wa Iringa ya kwanza ni Good Victory Primary School  iliyopo Manispaa ya Iringa  wastani 277.2344 nafasi ya pili The Glory Primary School  Iringa, wastani 270.4157 nafasi ya tatu Greenland Academy Primary School ya  Mufindi, wastani 265.2326 nafasi ya nne ni St Dominic Savio Mkim bizi Primary School – Iringa Manispaa ya Iringa kwa wastani 264.2247 nafasi ya tano pia ni St Dominic Savio Kigonzile Primary School  ya Maniapaa ya  Iringa kwa  wastani 258.4597  nafasi ya sita ni Camaldoli Primary School – Mafinga mji kwa  wastani 256.4808  huku nafasi ya saba ikienda Gangilonga Primary School ya Manispaa ya  Iringa kwa  wastani 254.069.

Na nafasi ya nane ikienda tena St Dominic Savio Primary School – Iringa Manispaa ya Iringa kwa wastani 253.9474 nafasi ya tisa 
Real Hope Primary School – Mafinga mji  wastani 253.8. nafasi ya kumi  ikienda Star Primary School  Iringa Manispaa ya Iringa kwa  wastani 242.4727.

JE, MTOTO WAKO ANASOMA SHULE IPI NA SHULE HIYO IMESHIKA NAFASI YA NGAPI KATIKA ORODHA HII?

Tuandikie kwenye sehemu ya maoni.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI