WAANDISHI mashuhuri wa michezo kimataifa, akiwemo bloga maarufu wa habari za Liverpool Haneefah, Sara Poraria kutoka televisheni maarufu ya Sporty nchini Hispania ambaye ameshahoji wachezaji nguli kama akina Ronaaldo, Jude Bellingham.
Pia yumo Alizee Morat, Cameron Corp maarufu kama “Freekick Specialist” na Adam Britton, wakiongozwa na Mtanzania John Jackson, mwandishi wa habari za michezo wa kimataifa, wamewasili nchini Tanzania, Oktoba 2, 2026, kwa ajili ya ziara ya kiutalii ya siku 8.
Ziara hiyo itawapeleka katika baadhi ya vivutio vya utalii nchini, ikiwemo Hifadhi za Taifa Serengeti na Ngorongoro, kwa lengo la kujionea kwa karibu uzuri, utajiri wa asili na vivutio vya Tanzania.
Baadhi ya Waandishi hao walishiriki katika kampeni ya kimataifa ya “Destination Tanzania” wakati wa Kombe la Dunia, ambapo walitumia majukwaa yao kuitangaza Tanzania kama moja ya vivutio bora vya utalii.
Kuelekea AFCON 2027, ziara hii pia inalenga kuwapa fursa waandishi hao kuona maandalizi na kuifahamu Tanzania kwa kina na kuendelea kuitangaza kupitia hadithi, picha na maudhui mbalimbali kwa hadhira ya kimataifa.
Akizungumza wakati wa chakula cha jioni na waandishi hao, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amesema ziara hiyo ni mwendelezo wa kampeni ya “Destination Tanzania” na hatua muhimu katika kuitangaza Tanzania kimataifa.
“Huu ni mwendelezo wa Destination Tanzania. Tumewapokea hawa na watakuwa na ziara ya siku 8 kuijionea uzuri wa Tanzania,” amesema Dkt. Abbasi.















0 Comments