Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mhe. Jackson Kiswaga amekabidhi mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Sadani, Kata ya Masaka, ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi aliyoitoa kwa wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi Mwenyekiti wa Kijiji cha Sadani Devis Msela amemshukuru Mbunge Kiswaga kwa kutimiza ahadi hiyo akisema msaada huo utasaidia kuongeza kasi ya ujenzi wa ofisi hiyo ulioanza mwaka huu.
Amesema kukamilika kwa ofisi hiyo kutakuwa suluhisho la changamoto zilizokuwa zikiwakabili viongozi wa kijiji, wakiwemo Mwenyekiti, Mtendaji na wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji kutokana na ofisi ya awali kutokuwa na ubora unaokidhi mahitaji ya kiutendaji.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Masaka amempongeza Mbunge Kiswaga akimtaja kuwa ni mbunge wa vitendo na kumshukuru kwa kuendelea kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.
Wananchi wa Sadani wameeleza kufurahishwa na kukamilika Kwa ahadi hiyo wakisema wana matumaini kuwa kukamilika kwa ofisi hiyo kutaboresha mazingira ya utendaji kazi wa viongozi wa kijiji na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.









0 Comments