Header Ads Widget

TETESI ZA SOKA JUMATANO ASTON VILLA WANATAKA KUMSAJILI ENDRIKIKWA MKOPO


Aston Villa iko tayari kufanya dili la kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Brazil, Endrick, mwenye umri wa miaka 20, baada ya kushindwa kumvutia kocha wa Real Madrid, José Mourinho.

Paris Saint-Germain na Liverpool wana nia ya kumsajili Rayan Cherki kutoka Manchester City, endapo kiungo huyo wa Ufaransa mwenye miaka 23 atawekwa sokoni.

Beki wa Ajax Mholanzi, Aaron Bouwman, mwenye miaka 19, yuko kwenye orodha ya wachezaji vijana wanaofuatiliwa na Newcastle kabla ya madirisha mawili yajayo ya usajili.

Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazomuwania kwa dhati kiungo mshambuliaji wa Mexico mwenye miaka 17, Gilberto Mora, anayekipiga Club Tijuana.

Bournemouth haina mpango wa kumuuza kiungo wa England Alex Scott, mwenye miaka 23, katika dirisha la Januari licha ya kuzivutia Chelsea pamoja na Real Madrid.Real Madrid imeshamfuatilia Alex Scott takribani mara tatu. Liverpool, Arsenal na AC Milan pia zinatajwa kuwa na shauku naye.

Beki wa Real Madrid, Antonio Rüdiger, mwenye miaka 33, anaonekana kuelekea kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu, huku Real Madrid ikiwa haina mpango wa kumpa mkataba mpya.

Tottenham itaweka kipaumbele katika kumsajili mshambuliaji katika dirisha la Januari, lakini huenda isitumie kiasi kikubwa cha fedha.

Real Madrid na Barcelona ziko tayari kumpa mchezaji chipukizi wa Manchester United, JJ Gabriel, mwenye miaka 15, mshahara mkubwa pamoja na bonasi na ada ya kusaini mkataba.

Bayern Munich bado ina matumaini ya kumsajili JJ Gabriel, lakini haitaki kukubali mshahara wa kiwango cha mamilioni unaodaiwa na upande wa mchezaji huyo.

Bayern Munich pia inamfuatilia mlinda lango wa Newcastle, Nick Pope, mwenye miaka 34, ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika msimu ujao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI