Header Ads Widget

TAMASHA LA MZIZIMA 2026 KUWA JUKWAA LA KUTANGAZA HISTORIA, UTAMADUNI NA FURSA ZA KIUCHUMI AFCON 2027



Tamasha la Mzizima 2026 linatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 11 hadi 13, mwaka huu katika Viwanja vya TTCL, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, likiwa na lengo la kuhifadhi na kutangaza historia ya mji wa Mzizima, utamaduni wa pwani pamoja na urithi wa jamii mbalimbali za mwambao wa Tanzania.

Tamasha hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Pamoja Tutashinda Tanzania (PATUTA), litabeba kaulimbiu isemayo “Mzizima Yetu, Utamaduni Wetu, Fursa Yetu”, likitarajiwa kuwakutanisha wananchi, wasanii, wafanyabiashara, wawekezaji na wadau wa utalii kupitia shughuli mbalimbali zikiwemo ngoma na muziki wa asili, vyakula vya asili, mavazi, michezo ya jadi na maonesho ya urithi wa utamaduni.

Aidha, tamasha hilo linalenga kukuza vipaji, kupanua masoko ya wasanii, kuhamasisha ujasiriamali kwa vijana na wanawake pamoja na kufungua fursa za biashara na uwekezaji, huku likiwa sehemu ya kuitangaza Tanzania kimataifa kuelekea mashindano ya AFCON PAMOJA 2027.

Waandaaji wamewaalika wananchi na wadau mbalimbali kujitokeza kushiriki, kuonesha bidhaa na vipaji vyao na kutumia fursa zitakazojitokeza kupitia tamasha hilo, ambalo pia linatarajiwa kuwa jukwaa la kuenzi historia na utambulisho wa Mzizima.












Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI