NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu nchini Israel uliofanyika Oktoba 27, 2026, yameacha nchi hiyo katika mkanganyiko wa kisiasa baada ya kambi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kushindwa kupata wingi wa viti bungeni (Knesset) ili kuunda serikali mpya.
Katika bunge hilo lenye jumla ya viti 120, chama cha Likud cha Netanyahu kikishirikiana na vyama washirika vya mrengo wa kulia vimefanikiwa kupata viti 53 pekee, idadi ambayo ni ndogo kuliko viti 61 vinavyohitajika kisheria kuanzisha serikali ya wengi.
Kambi kuu ya upinzani inayoongozwa na Gadi Eisenkot imejizolea viti 48, huku mshangao mkubwa ukijitokeza baada ya muungano wa vyama vya Waarabu, ukiwemo muungano wa The Joint List na Ra’am, kupata jumla ya viti 19.
Matokeo haya yanavipa vyama vya Waarabu nguvu kubwa ya maamuzi na ushawishi katika kuamua mustakabali wa kisiasa wa nchi hiyo.
MVUTANO NA TUHUMA ZA UDANGANYIFU
Muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, hali ya wasiwasi imeanza kutanda kufuatia kambi ya Netanyahu kuvishutumu vyama hivyo vya Waarabu kwa madai ya kufanya udanganyifu na kupokea uingiliaji wa kifedha kutoka mataifa ya nje.
Ripoti zinasema madai hayo yamepelekwa mbele ya shirika la usalama la nchi hiyo (Shin Bet) kwa ajili ya uchunguzi wa kina, ingawa nchi ya Qatar imekanusha vikali kuhusika na uingiliaji huo.
Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu Netanyahu ameweka wazi msimamo wake wa kukataa kata kata kushirikiana au kuunda serikali na vyama vya Waarabu, hatua inayozidisha ugumu wa kupata muungano thabiti wa kisiasa nchini humo.
HATMA YA SERIKALI YA ISRAEL YABAKI NJIA PANDA
Matokeo hayo yanaashiria kipindi kigumu cha mazungumzo ya kisiasa nchini Israel, huku vyama mbalimbali vikilazimika kutafuta ushirikiano ili kufikia idadi ya viti 61 inayohitajika kuunda serikali.






0 Comments