Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Mkuu wa mkoa Kigoma, Balozi Simon Siro amewataka wananchi wa mkoa Kigoma kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika mpango wa bima ya afya kwa wote awamu ya pili ambao utazinduliwa mkoani Kigoma Oktoba 21 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma Mkuu huyo wa mkoa alisemaa kuwa uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango huo wa bima ya afya kwa mkoa Kigoma utakaofanyika Oktoba 21 mwaka huu Zahanati ya Rusimbi Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma umelenga kuwafikia watanzania wote.
Balozi Sirro alisema kuwa awamu hii ya pili ya bima ya afya kwa wote inakuja baada ya kukamilika kwa mpango wa awamu ya kwanza uliokuwa unahusisha kaya masikini ambapo umetoa funzo kubwa kutokana na changamoto zilizojitokeza ambazo zimefanyika kazi kwa awamu hii ya pili.
Akitoa takwimu ya usajili ya awamu ya kwanza ya mpango huo Mkuu huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa Jumla ya kaya 11,454 wamesajiliwa kwa ajili ya kupata huduma za matibabu kupitia mpango huo kutoka kundi la kaya masikini ikiwa ni asilimia 76 ya lengo la kusajili kaya 15,037.
Balozi Siro alisema kuwa jumla ya watu 33,446 kutoka kwenye kaya hizo wamenufaika na mpango huo sawa na asilimia 51 ya watu 65,755 waliotarajiwa kunufaika na mpango kutoka kundi la kaya masikini na kwamba usajili kumalizia idadi ya watu waliobaki unaendelea.
Sambamba na hilo Mkuu huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa kupitia mpango wa Suzan Buffet jumla ya kaya 342 sawa na asilimia 33.9 zenye wanufaika 737 walihakikiwa na kupewa vitambulisho kati ya wanufaika 3031 waliokusudiwa.
kwa upande wake Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa Kigoma,Gwamaka Mwakyoma alisema kuwa usajili wa awamu ya pili ya mpango huo unataratayari kufanyika Oktoba 21 mwaka huu ambapo kuelekea uzinduzi huo NHIF imezifikia na kufanya uhakiki wa kaya 1264 zenye wanufaika 2028 ambao watapatiwa vitambulisho siku ya uzinduzi.
Meneja huyo wa NHIF mkoa Kigoma alisema kuwa zoezi la kwanza lilikuwa na majaribio ambapo kupitia mpango huo wamechukua changamoto zote na kuzifanyia kazi hivyo wanancho wote kuanzia sasa watafikiwa na huduma hiyo.


.jpeg)






0 Comments