Header Ads Widget

MAADILI YA WATOTO YANAANZIA NYUMBANI

Na Matukio Daima Media, Bagamoyo 

Wazazi na walezi wamehimizwa kuchukua nafasi ya kwanza katika ujenzi wa maadili ya watoto, wakielezwa kuwa msingi wa tabia unaojengwa nyumbani una mchango mkubwa katika aina ya jamii inayotarajiwa kuwa nayo hapo baadaye.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu Jeshi la Magereza, CP Ahmad Mwendad,wakati akizungumza  na wazazi na wanafunzi wa shule ya sekondari inayomilikiwa na Jeshi hilo ya Bwawani iliyopo Kijiji Cha Visakazi, katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze, Bagamoyo Mkoani Pwani.

Akawataka wazazi na walezi kutenga muda wa kukaa na watoto wao na kufuatilia mienendo yao badala ya kusubiri matatizo kujitokeza.

Amesema baadhi ya watoto wanaweza kuvutwa na makundi rika yenye ushawishi hasi iwapo wazazi watashindwa kufuatilia watu wanaoshirikiana nao, mienendo yao na mabadiliko yanayotokea katika maisha yao.

CP Mwendad amesema jukumu la malezi linapaswa kuanzia ndani ya familia, huku wazazi wakitakiwa kuwa mfano kwa watoto katika suala la nidhamu na maadili.

Kwa upande wao, wanafunzi na wazazi wamesema mtoto pia ana wajibu wa kutambua tofauti kati ya mwenendo unaojenga maisha yake na ule unaoweza kumuweka katika mazingira hatarishi.

Mwanafunzi 

Rebecca Moses na Kelvin Issac, wakasisitiza umuhimu wa kujenga tabia njema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI