Header Ads Widget

LISSU ATEULIWA HATUA YA MWISHO NA BUNGE LA ULAYA KATIKA TUZO YA SAKHAROV

Bunge la Ulaya limetangaza orodha ya wagombea watatu wa mwisho wa Tuzo ya Sakharov ya Haki za bindamu 2026, kwa kutambua mchango wao katika kutetea haki za binadamu, uhuru na demokrasia.

Walioteuliwa kufika hatua ya mwisho ni:

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na maafisa wake

Tundu Lissu wa Tanzania

Taraneh Rahimi na Romina Rahimi wa Iran

Tuzo ya Sakharov hutolewa kila mwaka kwa watu binafsi au mashirika yanayojitokeza kutetea haki za binadamu na uhuru wa msingi duniani kote.

Kila mwaka, Bunge la Ulaya hutunuku Tuzo ya Sakharov ya Uhuru wa Mawazo kwa watu binafsi au mashirika yanayoonyesha ujasiri wa kipekee katika kutetea haki za binadamu, demokrasia na uhuru wa msingi duniani.

Mwaka 2025, tuzo hiyo ilitolewa kwa Andrzej Poczobut, mwandishi wa habari na mwanaharakati wa jamii ya Wapolandi nchini Belarus, pamoja na Mzia Amaglobeli, mwandishi wa habari kutoka Georgia na mwanamke wa kwanza kutambuliwa kama mfungwa wa kisiasa nchini humo tangu taifa hilo lipate uhuru wake.

Kwa upande wa tuzo ya mwaka 2026, kamati za Mambo ya Nje na Maendeleo za Bunge la Ulaya zinatarajiwa kupigia kura orodha ya wagombea watatu wa mwisho tarehe 19 Oktoba mjini Strasbourg. Baadaye, Mkutano wa Marais wa Bunge la Ulaya utaamua mshindi wa tuzo hiyo tarehe 22 Oktoba 2026.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI