Header Ads Widget

KONGAMANO LA 49 KWA WAKUU WA HOSPITALI DUNIANI LAFUNGWA RASMI


Mkutano wa 49 wa Wakuu wa Hospitali Duniani (49th IHF World Hospital Congress 2026), ulioandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la Hospitali (IHF), umehitimishwa jijini Seoul, Korea Kusini, kwa msisitizo wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kukuza ubunifu na kuimarisha uwezo wa hospitali kukabiliana na mabadiliko katika sekta ya afya.

Akizungumza katika hafla ya kufunga mkutano huo, Rais wa IHF, Dkt. Henry Gallardo, alisisitiza kuwa mustakabali wa huduma za afya unategemea uwezo wa hospitali kubadilika, kushirikiana na kutumia ubunifu kuboresha huduma kwa wagonjwa.

Miongoni mwa masuala matano yaliyopewa kipaumbele ni matumizi salama na yenye maadili ya akili Unde (AI), uendelevu wa mazingira, usalama wa wagonjwa na wafanyakazi, uwekezaji katika maendeleo na ustawi wa wataalamu wa afya, pamoja na uendelevu wa kifedha wa hospitali.

Kongamano hilo limehimiza hospitali kutumia teknolojia kwa uwajibikaji, kusimamia rasilimali kwa ufanisi na kujenga mifumo imara inayoweza kukabiliana na majanga na changamoto za baadaye.

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Delilah Kimambo, MNH itaendelea kuwekeza katika Akili Unde (AI), uendelevu wa huduma bora na usalama kwa wagonjwa, utekelezaji wa mifumo madhubuti, mazingira bora ya kazi na ubunifu katika kuboresha huduma, ufanisi na miundombinu bora inayozingatia mahitaji ya wagonjwa.

Tanzania iliwasilishwa na wakuu wa hospitali kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya mifupa (MOI) na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH)




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI