Kambi maalum ya kuwafundisha wanawake matumizi ya silaha na utoaji wa huduma ya kwanza imeanzishwa mjini Tehran, huku viongozi wa Iran wakiendelea kuhimiza wananchi kuwa tayari "kuyatoa maisha yao kwa ajili ya kuilinda nchi."
Siku ya Jumapili, Uwanja wa Imam Hussein katika mji mkuu wa Tehran ulikuwa mwenyeji wa kambi hiyo ya kwanza ya aina yake inayowalenga wanawake.
Makumi ya wanawake walishiriki mafunzo hayo wakiwa wamevalia chador, vazi la kitamaduni linalofunika mwili mzima isipokuwa uso.
Hatua hiyo inakuja wakati mvutano ukiongezeka katika eneo la Mashariki ya Kati, huku bei za mafuta zikiendelea kupanda katika masoko ya kimataifa.
Iran imeapa kuendelea kuufunga Mlango wa Bahari wa Hormuz hadi Marekani itakapotekeleza masharti yake.
Maafisa wa Iran wanasema mafunzo hayo yanalenga kuwaandaa wananchi kukabiliana na hali za dharura na kuimarisha uwezo wa jamii kujilinda endapo kutatokea tishio kwa usalama wa taifa.
Hata hivyo, hatua hiyo imechukuliwa na wengi kama ishara ya maandalizi ya kukabiliana na mazingira ya mvutano unaoendelea katika kanda hiyo.







0 Comments