Header Ads Widget

BILIONI 3.1 ZALIPWA WALIOPISHA MRADI WA UMEME KIDAHWE

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

KIASI cha shilingi Bilioni 3.1 kimelipwa kwa wananchi 3424 waliopisha mradi wa ujenzi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme wa msongo wa kilo Volt 44 katika eneo la Kidahwe wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.

 

Msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Ramadhani Kidunda alisema hayo akitoa taarifa kwa Katibu Tawala wa mkoa Kigoma,Hassan Rugwa aliyefanya ziara kutembelea mradi huo ambapo alisema kuwa idadi hiyo ni kati ya watu 3612 waliofanyiwa uthamini na kuidhinishwa kwa ajili ya malipo hayo.

 

Mhandisi Kidunda alisema kuwa watu 188 mpaka sasa  hawajalipwa kutokana na kutokamilisha nyaraka mbalimbali zikiwemo za masuala ya mirathi na vitambulisho na kwamba fedha zao zipo na pindi watakapokamilisha nyaraka hizo malipo yao yatafanyika.

 

Akitoa taarifa ya  mradi wa kituo cha kupoza umeme Kidahwe na kusafirisha umeme wa Msongo wa Kilo Volt 400 kutoka Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera Msimamizi huyo alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo unaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 164.8 unakwenda vizuri na kwa sasa  umefikia asilimia 60 na unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

 


Akizungumza baada ya kutekeleza mradi huo Katibu  Tawala wa mkoa Kigoma, Hassan Rugwa alieleza kuridhishwa na hatu za utekelezaji wa miradi hiyo baada ya changamoto zilizokuwepo awali kufanyiwa kazi na kwamba wametoa maelekezo kwa Msimamizi wa mradi Shirika la Uzalishaji na ugavi wa umeme (TANESCO) kumsimamisi Mkandarasi kwa karibu na kutoa taarifa mapema kila inapojitokeza changamoto.

 

Pamoja na hivyo Katibu Tawala huyo wa mkoa Kigoma amesema kuwa miradi hiyo inaufanya mkoa Kigoma kuwa na kiasi kikubwa cha umeme na ziada ya kuttosha hivyo amewataka wawekezaji wanaotaka kuja mkoani humo kwa ajili ya uwekezaji kwenye viwanda kutokuwa na wasiwasi na upatikanaji wa umeme.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI