Na Matukio Daima Media, Dar es salaam.
KAMPUNI ya Zara Tanzania Adventures imefanikiwa kuzindua msimu wa tano wa kampeni ya "Twenzetu kileleni 2026" Ikiwa na lengo kuu kupanda mlima Kilimanjaro na kusheherekea miaka 65 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania).
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi uliofanyika leo September 10, 2026 katikaChuo cha Taifa cha Utalii (National College of Tourism), Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Zara Tanzania Adventure, Bi. Zainabu Ansell (Mama Zara) amesema kampeni hiyo inatarajiwa kuwashirikisha zaidi ya Watalii 200 mwaka huu, wote wakipanda Mlima Kilimanjaro kwakupitia njia ya Marangu kwa ajili ya kusherekea Uhuru, 9 Desemba.
Mama Zara amesema msimu wa Tano, ikiwa na dhamira ya kuhamasisha Watanzania kusafiri, kugundua na kujivunia utajiri wa asili na vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania ambapo watapanda kwa bei nafuu kwa kiwango Cha Tsh 1.800.000 (Milioni Moja laki Nane) ambapo imejumlisha vitu vyote malazi, chakula, vifaa, usafiri na tozo Serikali.
Zoezi hilo la kupanda Mlima Kilimanjaro linatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 5 hadi Desemba 10, 2026, likiwa pia ni sehemu ya kuendelea kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, hususani Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Aidha, mbali ya kuzindua twenzetu kileleni msimu wa Tano, ZARA pia wamezindua Twenzetu Serengeti kwa matukio ya Utalii msimu mzima wa December.
Tutakuwa na safari ya kuanzia Springlands hotel Mjini Moshi, kwa gharama ya Tsh 1,200,000 (Milioni 1.2), gharama kwa kila mtu, safari ya siku Nne.
"Twenzetu Serengeti itajumlisha usafiri wa Land cruiser 4x4, chakula,vinywaji laini, malazi, viingilio vya Hifadhi. Kwa wageni kila gari watu 7.".
Kwa upande wao baadhi ya wadau:
Afisa Tehama wa TTCL, Peter Mwambungu amesema TTCL wanaendelea kuboresha Mawasiliano na watu wote wanaoenda kileleni kufurahia huduma nzuri ya Mawasiliano simu na huduma ya intaneti wakati wote wawapo kileleni.
Nae Gilda Swali kutoka kampuni ya bima ya BUMACO amesema wanaungana na Zara ambapo pia wapanda mlima watapata huduma ya bima.
Kwa upande wake, Meneja uhamasishaji uwekezaji kutoka TISEZA, Daudi Liganda amesema TISEZA inaunga mkono juhudi za kampuni hiyo ambayo imewekeza kwenye Sekta ya Utalii
"Sisi TISEZA mwaka huu tutaungana na zara kupanda kilelelni kwani siyo mara ya kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro kwani tumepanda mwaka 2021 hivyo tunataka kuiambia Dunia kwamba Tanzania ni mahali salama kwa uwekezaji hivyo watu waje kuwekeze ; amesema Liganda
Katika uzinduzi huo wadau mbalimbali wameweza kushiriki akiwemo Bodi ya Utalii (TTB), kampuni ya simu ya TTCL, TISEZA, kampuni ya bima ya BUMACO, MSD, Chuo cha Utalii cha Taifa, na wengine wengi.
Mwisho








0 Comments